Kampuni za China zina imani ya kushinda changamoto na kutimiza maendeleo endelevu
2020-02-10 19:14:41| CRI

Hivi karibuni kampuni nyingi za China zilianza tena uzalishaji. Baraza la serikali la China lilitoa taarifa likisisitiza kuimarisha kukinga na kuzuia maambukizi ya virusi vipya vya korona kwa njia ya kisayansi, na kushughulikia kwa utaratibu kazi ya uzalishaji ya kampuni. Katika hali hii ya maambukizi, kampuni za China zinatafuta njia mpya za ongezeko na kupanua fursa mpya za maendeleo

Namna ya kupunguza athari ya maambukizi kwa kampuni imekuwa suala linalofuatiliwa sana kwa uchumi wa China. Wakati wa kukinga na kuzuia maambukizi ya virusi vya korona, kampuni mbalimbali za China zinafanya juhudi kuanza tena uzalishaji, na zimeonesha uwezo mkubwa wa kujiboresha. Wakati huo huo, serikali ya China pia imerekebisha sera na kuunga mkono uzalishaji wa kampuni.

Kutokana na msingi mzuri wa uchumi, kampuni za China zina imani ya kukabiliana na changamoto na kutimiza maendeleo endelevu. Hivi sasa wanauchumi wengi wa ndani na nje ya nchi wameona kuwa, ingawa hali ya maambukizi imeathiri uchumi wa China, lakini athari hiyo ni ya muda mfupi. Mazingira ya kimsingi ya maendeleo yenye sifa ya juu ya uchumi wa China hayatabadilika, na mwelekeo wa ongezeko la uchumi wa China hautabadilika. Ukweni ni kwamba, China ina soko kubwa la watu bilioni 1.4, na mfumo wa dunia uliokamilika wa mnyonyoro wa viwanda na ugavi, miundombinu bora, na idadi kubwa ya wanateknolojia, ni msingi imara wa maendeleo ya uchumi wa China, pia ni nguvu kubwa ya kuhimiza maendeleo ya kampuni.

Kampuni za China hupata maendeleo wakati wa kukabiliana na changamoto. Kwa uwezo mkubwa wa kujiboresha, uungaji mkono wa serikali, msingi imara wa uchumi, kampuni hizo hakika zitashinda matatizo ya muda, kupata maendeleo mapya, na kutia nguvu katika ongezeko la uchumi wa China.