Wakati wa taabu, kuwasaidia wengine ni kama kujisaidia mwenyewe
2020-02-26 21:07:11| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, kuwasaidia watu wanaoisaidia China ni desturi ya kijadi ya China, na nchi hiyo inaishukuru jamii ya kimataifa kwa kuiunga mkono katika kupambana na COVID-19.

Katika tahariri yake iliyopewa kichwa cha "Wakati wa taabu, kuwasaidia wengine ni kama kujisaidia mwenyewe", Shirika Kuu la Utangazaji la China limesema, tangu kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 nchini China, viongozi wa nchi zaidi ya 170 na mashirika zaidi ya 40 ya kimataifa wameiunga mkono China katika vita dhidi ya ugonjwa huo, na baadhi yao zikiwemo nchi za Afrika zimetoa misaada halisi.

Wakati huohuo, China imetoa uzoefu wa kupambana na COVID-19 na misaada kwa nchi nyingine zinazoathiriwa. Rais Xi Jinping wa China pia ameahidi kuendelea kutoa misaada ya vifaa na dawa kwa nchi za Afrika, ili kukabiliana na matishio ya COVID-19.