Kauli zisizo za kweli za Pompeo na Marekani zinavyokosa mwelekeo
2020-02-27 21:25:36| CRI

Watu wa Marekani wanaona, kila mwanasiasa ana nembo yake. Katika nafasi ya waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Henry Kissinger anajulikana kwa busara zake za kushughulikia mambo ya diplomasia, na Mike Pompeo huenda atakumbukwa na watu kutokana na kauli zake zisizo za ukweli.

Katika mkutano wa usalama uliofanyika hivi karibuni mjini Munich, Ujerumani, Pompeo alisema, uhusiano wa nchi washirika kati ya Marekani na Ulaya haujakwisha, na nchi za Magharibi zinakaribia ushindi wa pamoja. Kuhusu kauli hiyo, makala iliyotolewa na gazeti la The Guardian la Uingereza halikuzungumzia ushindi wa pamoja wa Marekani na Uingereza, bali lilisema nchi hizo zinapingana kwa vitendo, msimamo tofauti katika suala la teknolojia ya 5G ya Huawei, ni kasoro mpya kati ya washirika hao wawili. Makala hiyo inadokeza kuwa, mkutano wa viongozi wa Marekani na Uingereza uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Machi mjini Washington umefutwa.

Uingereza imekubali Huawei ijiunge na mradi wa ujenzi wa mtandao wa 5G nchini humo, jambo ambalo linathibitisha kuwa teknolojia ya kampuni hiyo ni salama na ya kuaminika. Hata hivyo, Marekani inaendelea kutumia kila iwezalo ikilenga kuzuia na hatimaye kuangamiza kampuni za teknolojia ya juu za China, ikitumia mbinu za kuharibu maslahi ya washirika wake. Makala hiyo inasema, umwamba na ujeuri wa Marekani, pamoja na shinikizo lake katika mazungumzo ya makubaliano ya kiuchumi ni changamoto kubwa kwa Uingereza.

Pia uhusiano kati ya Marekani na Ulaya pia uko utatani. Ili kutimiza lengo la "Marekani Kwanza", serikali Marekani imetumia silaha ya kuongeza ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za Ulaya. Katika mambo ya kisiasa, Marekani inaendelea na juhudi za kuvunja muungano wa nchi za Ulaya. Kiusalama, Marekani ilijitoa katika makubaliano ya kuzuia makombora ya masafa ya kati, yaliyosainiwa miaka 30 iliyopita kati yake na Russia kwa ajili ya kuondoa tishio la mabomu ya nyuklia dhidi ya Ulaya.

Kwa maoni ya serikali ya sasa ya Marekani, nchi nyingine zote duniani zinajinufaisha kwa kutumia Marekani, ndio maana serikali hiyo inafanya kila juhudi kuvunja utaratibu uliopo wa kisiasa na kiuchumi duniani. Kama Pompeo alivyosema katika hotuba yake, "tunasema uwongo, tunadanganya, tunaiba."