Marekani yahofia mchina kugombea nafasi ya mkuu wa shirika la UM
2020-02-28 19:53:13| CRI

Uchaguzi wa mkurugenzi mkuu wa Shrika la Haki Miliki za Ubunifu Duniani WIPO utafanyika wiki ijayo mjini Geneva, Uswisi, na nchi mbalimbali ikiwemo China zimependekeza wagombea wao kwa ajili ya nafasi hiyo. Lakini hivi karibuni, baadhi ya wanasiasa wa Marekani wamefanya tena mchezo wao wa kisiasa.

Kwa mfano, timu ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo iliikashifu China kwa "kuiba haki miliki za ubunifu", na kudai kuwa "ni kichekesho kuiruhusu China kuongoza chombo hicho kinachosaidia kutunga sera za haki miliki za ubunifu za kuvuka mipaka ya nchi'. Hata Marekani imetoa shinikizo kwa nchi nyingine ikizitaka zisimpigie kura mgombea wa China na kusema "ni sawa kwa mtu yeyote isipokuwa mchina"

Je, Marekani inaogopa nini na kufanya kila iwezalo kumzuia mchina kugombea nafasi hiyo?

WIPO ni shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia kulinda haki miliki za ubunifu za nchi mbalimbali, na muda wa mkurugenzi mkuu wake kuwa madarakani ni miaka sita, na nchi zote wanachama zina haki ya kupendekeza wagombea.

Tangu China ijiunge na Shirika hilo tarehe 3, Juni mwaka 1980, imekuwa ikiimarisha ulinzi wa haki miliki za ubunifu na ushirikiano wa kimataifa. Kama alivyosisitiza rais Xi Jinping wa China, kuimarisha ulinzi wa haki miliki za ubunifu sio tu ni sehemu muhimu katika kukamilisha utaratibu wa kulinda haki miliki za ubunifu, bali pia ni hamasa kubwa ya kuongeza nguvu ya ushindani ya uchumi wa China. Kwa mujibu wa viashiria vya ubunifu duniani kwa mwaka 2019 vilivyotolewa na WIPO, China ilipanda kwa miaka minne mfululizo na kufika nafasi ya 14.

Mkurugenzi mkuu wa sasa wa WIPO Francis Gurry amesema China imejitahidi kushiriki kwenye mikutano, miradi na uanzishwaji wa mifumo ya shirika hilo, hatua ambayo inaunga mkono utaratibu wa ulinzi wa haki miliki za ubunifu duniani, na sauti ya China inakuwa sauti muhimu ya utaratibu wa sera duniani. Amesisitiza kuwa kumpendekeza mgombea wa nafasi ya mkurugenzi mkuu wa WIPO kumeonesha nia nzuri ya China ya kuchangia ushirikiano na maendeleo ya haki miliki za ubunifu duniani.

Mgombea aliyependekezwa na China Bi. Wang Binying sasa ni naibu mkurugenzi mkuu wa WIPO, na amelifanyia kazi shirika hilo kwa miaka karibu 30, ametambuliwa kama ni mgombea mwenye uzoefu mkubwa, uwezo mkubwa na nguvu kubwa ya ushindani.

Kutoka mchango wa nchi hadi uwezo wa mgombea, China iko wazi na inafuata kanuni husika. Lakini Marekani, mbali na kutopendekeza mgombea wake, pia imepuuza kanuni na kuchafua jina la China vibaya. Hiki ndicho kitendo cha mtu anayefuata vigezo viwili na sera ya umwamba.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imejitoa kwenye mashirika mengi ya kimataifa, na mara nyingi ilichukua hatua za upande mmoja bila kujali maamuzi ya Umoja wa Mataifa. Kwa upande mwingine, imechelewa kulipa ada ya uanachama ya Umoja wa Mataifa, kuzuia mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Shirika la Biashara Duniani WTO kutenda kazi zake za kawaida, na imeharibu utaratibu wa kimataifa na ushirikiano wa pande nyingi.

Safari hii, Marekani imenyoosha mkono wake kwa uchaguzi wa WIPO na hata kulazimisha baadhi ya nchi kuacha kumwunga mkono mgombea wa China kwa kutishia kusimamisha misaada. Hii imeonesha fikra sugu ya vita baridi na wazo la vita walilo nalo baadhi ya wanasiasa wa Marekani, ambao hawawezi kukubali nchi kama China kupata maendeleo.

Uchaguzi wowote unatakiwa kufanywa kwa haki na usawa, bila kusema huu ni uchaguzi wa msimamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa. Marekani imekwenda mbali kwa kufanya uchaguzi huu kuwa "mchezo wa kisiasa" kwa ajili ya maslahi yake binafsi. China inaamini kuwa nchi zote zitapiga kura kwa kujiamulia kwa kufuata fikra zao na malshi yao yenyewe, wala sio kujisalimu kwa shinikizo lisilo la maadili la Marekani.