Kwa nini utabiri wa "kuporomoka kwa China" imevunjwa tena?
2020-02-29 20:06:05| CRI

Katika miongo kadhaa iliyopita, kutokana na ubaguzi wa kisiasa, baadhi ya wasomi na wanahabari wa nchi za magharibi mara nyingi wamekuwa wakitabiri kuwa "China itaporomoka", lakini utabiri wao huvunjwa kila mara. Baada ya mlipuko wa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya ya korona COVID-19, watu hao wametabiri tena kuwa, China itaporomoka kutokana na ukosefu wa uwezo wa kutosha wa kukabiliana na ugonjwa huo. Lakini utabiri huo umevunjwa tena.

Licha ya mkoa wa Hubei, kesi mpya za maambukizi ya COVID-19 katika sehemu nyingine nchini China jana zilipungua na kuwa nne tu, na viwanda vimerejesha uzalishaji kwa utaratibu. Wakati huohuo kikundi cha pamoja cha wataalamu wa China na Shirika la Afya Duniani WHO baada ya kufanya ukaguzi kimetoa ripoti na kusema, kwa kuchukua hatua madhubuti, na zenye ujasiri na ufanisi zaidi, China imefanikiwa kukatisha njia ya maambukizi ya COVID-19, na kutoa uzoefu muhimu kwa jamii ya kimataifa kukabiliana na ugonjwa huo.

Hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China mara nyingi amekuwa akisisitiza mawazo ya jumuiya yenye hatma ya pamoja, na kusema mshikamano ni silaha yenye nguvu zaidi katika kukabiliana na ugonjwa unaotishia usalama wa afya ya binadamu wote. Katika kipindi hiki muhimu cha kupambana na COVID-19, kitendo cha kuipaka matope China na kufanya juhudi zake za kuzuia virusi ziwe suala la kisiasa hakiwezi kuleta ushindi dhidi ya virusi, badala yake, kitasababisha kukosa fursa ya kupata ushindi huo.