Tishio la usalama wa afya duniani halipaswi kugeuzwa mchezo wa kisiasa
2020-03-02 19:47:37| CRI

Zaidi ya nchi 60 duniani zimekumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya ya korona COVID-19, na Shirika la Afya Duniani WHO limeinua kiwango cha tishio la ugonjwa huo duniani kuwa "juu sana".

Ikiwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya COVID-19, China imefanya juhudi kubwa, na imepata ufanisi mzuri, China pia imetoa misaada kwa nchi nyingine zinazokumbwa na ugonjwa huo.

Wakati huohuo, baadhi ya wanasiasa wa nchi za magharibi wametoa habari zisizo za kweli kuhusu vita ya China dhidi ya virusi vya korona. Hivi karibuni, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amekosoa juhudi za China za kukabiliana na maambukzi ya virusi, na kupaka matope mfumo wa kisiasa wa China, na kuilaumu China bila kujali hali halisi na maoni ya pamoja ya jamii ya kimataifa.

Virusi havijali mipaka. Katika kipindi hiki muhimu cha vita dhidi ya COVID-19, kuacha ubaguzi, kuvunja hali ya kutengana, kujifunza, kushikamana na kushirikiana ndio njia pekee ya kushinda vita hiyo.