China yafafanua wazo la jumuiya yenye hatma ya pamoja kwa vitendo halisi
2020-03-03 19:57:36| CRI

"Nawashukuru Wachina wote wanaoishi maisha yasiyo ya kawaida, wameacha mambo ya kujifurahisha, kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi. Huu ni mchango mkubwa kwa binadamu wote duniani."

Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Hadi sasa zaidi ya nchi 60 duniani zimeathiriwa na maambukizi ya ugonjwa wa nimonia unaosababishwa na virusi vipya vya korona (COVID-19). Wakati jamii ya kimataifa inapokabiliana na ugonjwa huo, pia imetambua vizuri zaidi juhudi za China za kulinda usalama wa afya ya umma.

Baada ya kutokea kwa mlipuko wa COVID-19, rais Xi Jinping wa China ametaja mara nyingi wazo la jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kusisitiza China si kama tu inawajibika na usalama wa maisha na afya wa wananchi wake, bali pia inawajibika na usalama wa afya wa watu wote duniani. Ili kufanya hivyo, kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita, China imechukua hatua kali zaidi, na kufanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi. Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani WHO wamepongeza hatua hizo za China, na kusema kutokana na hatua hizo, malaki ya watu wameepuka kuambukizwa na virusi hivyo.

Wakati huohuo, China pia imezisaidia nchi nyingine kupambana na ugonjwa huo. Kwa mfano, kwa kushirikiana na WHO, China imezisaidia nchi za Afrika kujenga uwezo wa kukagua virusi vipya vya korona. Pia imetuma kikundi cha wataalamu wa kujitolea nchini Iran, ambayo pia imeathiriwa sana na COVID-19, aidha, China pia imetoa misaada kwa Japan na Korea ya Kusini.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Bill and Melinda Gates Bill Gates amesema, kwa kukabiliwa na utatanishi wa maambukizi ya virusi, mshikamano na ushirikiano unapaswa kuwa kanuni ya kimsingi kwa nchi zote duniani.

Juhudi za China kupambana na COVID-19 si kama tu ni kwa ajili ya kulinda afya ya wananchi wake, bali pia ni nguvu kubwa ya kuunga mkono juhudi za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huo. Ikiwa nchi kubwa inayowajibika, China imepata uzoefu mkubwa unaoweza kuigwa na jamii ya kimataifa katika mapambano hayo.

Virusi havijali mipaka, na dunia nzima inakabiliwa na changamoto ya pamoja. Wakati huo, jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja ina maana halisi zaidi kuliko wakati mwingine wowote. China inatekeleza ahadi yake ya kujenga jumuiya hiyo kwa vitendo halisi.