Jamii ya kimataifa haitatishwa na mswada wa Marekani kuhusu Taiwan
2020-03-09 17:23:41| CRI

Wakati dunia inakabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanalihimiza baraza la chini la bunge la nchi hiyo kupitia "mswada wa mwaka 2019 kuhusu Taipei", ambao unaitaka serikali ya Marekani irekebishe uhusiano kati yake na nchi nyingine zinayorekebisha sera yake kuhusu Taiwan, ili kuiunga mkono Taiwan kuongeza nafasi ya kisiasa duniani.

Zaidi ya miaka 40 iliyopita, Marekani ilianzisha uhusiano wa kibalozi na China kwa mujibu wa kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani. Kwa nini sasa inazuia nchi nyingine kuanzisha uhusiano wa kibalozi na China? Sababu halisi ni kwamba Marekani inataka kuvuruga maendeleo ya China kupitia suala la Taiwan.

Tangu Cai Yingwen awe madarakani, nchi 7 zimevunja uhusiano wa kibalozi na Taiwan, na kuanzisha au kurejesha uhusiano rasmi na China. Hali hii inaonesha kuwa kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani ni maoni ya pamoja ya jamii ya kimataifa.

Mwezi Agosti mwaka 2018, wakati El Salvador ilipokuwa ikitaka kuvunja uhusiano wa kibalozi na Taiwan, John Bolton aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa la Marekani alimpigia simu rais Salvador Sanchez Sellen wa El Salvador, na kumwonya asifanye hivyo. Lakini El Salvador ilipuuza shinikizo la Marekani, na kuanzisha uhusiano wa kibalozi na China. Aidha, mwaka jana, makamu wa rais wa Marekani Mike Pence pia alishindwa kuvishawishi Visiwa vya Solomon kutovunja uhusiano wa kibalozi na Taiwan.

Ni dhahiri kwamba kurejesha au kuanzisha uhusiano wa kibalozi na China ni mwelekeo wa siasa ya kimataifa, ambao Marekani haiwezi kuuzuia. Mswada wa mwaka 2019 kuhusu Taipei unakiuka sheria na kanuni ya kimataifa, na hauna msingi wowote wa kisheria, hauwezi kuitishia jamii ya kimataifa inayoshikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani, na pia hautavuruga maendeleo ya China.

Hadi sasa nchi 180 duniani zimeanzisha uhusiano wa kibalozi na China, na China inazitendea nchi zote kwa usawa, bila kujali ukubwa, nguvu na utajiri wake.

Kwa upande wa Taiwan, maslahi yake inahusiana na umoja na ustawi wa taifa la China. Wanasiasa wa Marekani hawajali maslahi ya Wataiwan, na wanataka kuzuia tu maendeleo ya China.

Suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya China, na linahusiana na maslahi kuu ya China. Baadhi ya wanasiasa wa Marekani kuchochea mswada kuhusu Taiwan hakutabadili mchakato wa umoja wa China. China inaitaka Marekani isipitie mswada huo, ili isilete matatizo zaidi kwa uhusiano kati ya nchi hizo.