Marekani yashindwa kutumia fursa ya kukabiliana na COVID-19 iliyotokana na juhudi za China
2020-03-10 20:09:44| CRI

Kesi mpya za maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona (COVID-19) nchini China zimepungua na kufikia chini ya 20 hapo jana, na kulifanya Shirika la Afya Duniani kusema, maambukizi ya ugonjwa huo nchini China yanamalizika.

Wakati huohuo, wagonjwa wa COVID-19 nchini Marekani wanaendelea kuongezeka, na hadi saa 1 jioni ya tarehe 9, kesi za maambukizi ya ugonjwa huo zilifikia 704, na wagonjwa 26 wamefariki.

Ikiwa nchi yenye kiwango cha juu zaidi cha matibabu, kuzuia ugonjwa huo isingekuwa tatizo kubwa. Tarehe 20 Januari, Marekani iligundua mgonjwa wa kwanza, lakini serikali ya nchi hiyo haikuwa na wasiwasi na kusema watu wanaweza kukabiliana na ugonjwa huo kama mafua. Msimamo huo wa serikali ya Marekani umechelewesha juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo. Gazeti la New York Times limesema, serikali ya Marekani imefanya makosa mbalimbali, ikiwemo kutotoa habari kwa uwazi, kuzingatia zaidi siasa na kukosa ufanisi.

Mwenyekiti wa Shirika la Afya la ACCESS William Haseltine amesema, kama Marekani ingechukua hatua mwafaka kabla ya mlipuko wa ugonjwa, hali ingekuwa nzuri kuliko sasa.