Baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanavuruga ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na COVID-19
2020-03-20 19:28:08| CRI

Maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 yanaenea kwa kasi duniani, na jamii ya kimataifa inahitaji kuimarisha ushirikiano ili kushinda janga hili, lakini baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanavuruga ushirikiano huo kufuatia vitendo vyao vya kibinafsi.

Habari zilizotolewa na Shirika la Utangazaji la Colombia la Marekani zinasema, mkurugenzi wa kamati ya biashara ya Ikulu ya Marekani Peter Navarro amemtaka rais wa Marekani kutoa amri ya kurudisha makampuni ya dawa na vifaa vya tiba ya nchi hiyo kutoka nchi za nje, ili kukidhi mahitaji ya ndani. Wakati huohuo, serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola bilioni moja kwa kampuni moja ya Ujerumani inayotafiti chanjo dhidi ya virusi vya Corona, ili kuhakikisha chanjo hiyo inatolewa kwa Wamarekani tu. Vyombo vya habari vya Ujerumani vimelaani vikali kitendo hicho, na kusema Marekani imeonesha uovu wake kwa jamii ya kimataifa.

Kutokana na mawazo ya baadhi ya wanasiasa wa Marekani, vitendo vya kujilinda na "Marekani kwanza" ni jambo la lazima, na wameharibu ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na COVID-19.