Hivi karibuni baadhi ya Wamarekani wanavitaja virusi vya Corona kuwa ni "virusi vya kichina", hali ambayo imelaumiwa na jumuiya ya kimataifa.
Chanzo cha virusi ni suala la kisayansi ambalo linahitaji kuthibitishwa kwa njia ya kisayansi. Hivi karibuni mtaalamu mashuhuri wa matibabu wa Italia Bw. Giuseppe Remuzzi alisema, kuna uwezekano kuwa nimonia inayofanana sana na ile inayosababishwa na virusi vya Corona COVID-19 ilianza kutokea mwezi Novemba na Disemba mwaka jana nchini humo, hali ambayo inaonesha kuwa kabla ya maambukizi ya virusi vya Corona kulipuka nchini China, virusi hivyo vilikuwa vimeenea kwenye eneo la Lombardia.
Kauli hii inathibitisha tena maoni ya mtaalamu wa magonjwa ya pumu wa China Bw. Zhong Nanshan kuwa, kuna uwezekano kuwa mlipuko wa virusi vya Corona haukuanzia China. Mwandishi wa habari wa Uingereza Amanda Walker pia amedhihirisha kuwa, endapo mamilioni ya Wamarekani watafariki, rais anatakiwa kuwajibika, na kuvitaja virusi hivyo kuwa "virusi vya kichina" ni njia ya kuepuka lawama.
Waziri mkuu wa Australia Bw. Scott Morrison hivi karibuni alipofanyiwa mahojiano amesema asilimia 80 ya wagonjwa wa Corona waliothibitishwa nchini humo wanatoka nje ya nchi au kuwasiliana na watu waliorudi kutoka nchi za kigeni, na wengi wao wanatoka Marekani.
Kutokana na mashaka mengi dhidi ya Mareknai, serikali ya Marekani inapaswa kutoa maelezo wazi kuhusu masuala matatu:
Kwanza, kwa mujibu wa takwimu kutoka Kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Marekani, mlipuko wa homa ya mafua uliotokea mwezi Septemba mwaka 2019, umesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 20. Mkurugenzi wa kituo hicho amekiri baadhi ya watu walifariki kutokana na virusi vya Corona. Je, kati ya vifo vya watu hao elfu 20, vifo vingapi vilitokana na virusi vya Corona. Je Marekani imeficha hali halisi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa kutumia homa ya mafua?
Suala la pili ni kwa nini Marekani ilifunga kwa dharura kituo cha silaha za kikemikali kilichoko huko Fort Detrick, jimbo la Maryland mwezi Julai mwaka jana. Kituo hicho ni kituo kikubwa zaidi cha jeshi la Marekani cha kutafiti na kuendeleza silaha za kikemikali. Sababu halisi ya kufungwa kwa kituo hicho ilitiliwa mashaka na watu kwani kesi za nimonia zilianza kutokea nchini humo. Wakati huo huo, homa ya mafua H1N1 ililipuka nchini Marekani, mwezi Oktoba mashirika mengi ya Marekani yalianzisha mazoezi ya magonjwa ya kuambukiza duniani, mwezi Disemba mgonjwa wa kwanza wa virusi vya Corona alitokea mjini Wuhan, mwezi Februari mwaka huu maambukizi ya virusi vya Corona yakaenea katika sehemu mbalimbali duniani. Je, matukio hayo ya ajabu yana uhusiano wowote?
Suala la tatu ni kuwa, kwa nini serikali ya Marekani ilificha hali halisi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo katikati ya mwezi Februari, wakati maofisa wengi wa upelelezi wa baraza la juu la bunge waliuza hisa zenye thamani ya mamilioni ya dola za kimarekani? Kwa nini wanasiasa wanauza hisa kwa kutumia habari za siri huku wakificha hali halisi ya ugonjwa? Kwa nini wanazingatia mali zaidi kuliko maisha?
Gazeti la Washington post limeripoti kuwa, maofisa wa upelelezi wa Marekani walitoa onyo mara nyingi mwezi Januari mwaka huu, kuwa virusi vya Corona vinaweza kuleta migogoro duniani, na kusisitiza ulazima wa hatua za serikali. Lakini serikali ya Marekani ilitangaza kuingia kwenye "hali ya dharura" hadi tarehe 13 Machi. Kwa nini Marekani inatumia ovyoovyo muda muhimu wa kuzuia ugonjwa ambao uliokolewa na China kwa kupata hasara kubwa?
Wanasiasa wanatakiwa kutoa maelezo wazi kwa mashaka hayo.
Muda na maisha ya watu haviwezi kurudishwa. Endapo baadhi ya wanasiasa wa Marekani hawajikosoi mapema, hakika watapata hasara kubwa.