Mswada wa Marekani kuhusu Taiwan wadhuru pande zote wakati dunia inakabiliana na COVID-19
2020-03-28 19:34:45| CRI

Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 26 alisaini mswada wa mwaka 2019 kuhusu Taibei na kuufanya uwe sheria, ili kuzuia nchi nyingine kuanzisha uhusiano wa kibalozi na China. Mswada huo unakiuka kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, na kwenda kinyume na uhusiano na kanuni za kimsingi duniani, pia utasumbua juhudi za kimataifa za kukabiliana na COVID-19. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Mswada wa Marekani kuhusu Taiwan wadhuru pande zote wakati dunia inakabiliana na COVID-19".

Tahariri hiyo inasema, kama miswada mingine iliyotolewa na Marekani, mswada huo unalenga kuunga mkono wafarakanishaji wa Taiwan kwa kuimairisha uhusiano wa kibalozi kati ya Taiwan na nchi chache zinazobaki. Wakati dunia inakabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, mswada huo utaharibu ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na virusi hivyo, haswa ushirikiano kati ya China na Marekani.

Suala la Taiwan ni maslahi makuu ya China. Kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani, na pia ni maoni ya pamoja ya jamii ya kimataifa. Miswada kama hiyo kuhusu Taiwan si kama tu itaharibu uhusiano kati ya China na Marekani, bali pia itadhuru maslahi ya Marekani.