Moyo wa dhati haupaswi kuchafuliwa kwa nia mbaya ya kisiasa
2020-03-31 20:08:29| CRI

Wakati vifaa vya matibabu vya China vinapofika katika nchi za nje, baadhi ya watu wa magharibi wanatoa kauli za uchochezi kwa kusema China inatoa msaada wa kupambana na virusi vya Corona ili kuongeza ushawishi wake duniani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying alisema China haiwezi kukaa bila kufanya kitu wakati nchi nyingine zinaathiriwa vibaya na virusi vya corona.

Nchi zaidi ya 200 duniani zimeripoti maambukizi ya virusi vya corona, ambayo yamefikia zaidi ya laki nane, na katika kipindi hicho, China inashirikiana na nchi hizo na kutoa msaada kadri iwezavyo. Hata hivyo baadhi vyombo vya habari vya magharibi vimechafua moyo wa dhati wa China na kuchochea uadui kati ya China na nchi zinazopokea msaada.

Lakini China ina lengo moja tu kwa kuzisaidia nchi nyingine kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, kuokoa maisha ya watu, na kutafsiri hatua hizo kwa njia ya kisiasa kunaweza kuharibu ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na virusi hivyo.

Janga hilo linaloishambulia ghafla dunia limethibitisha kwa nguvu kuwa binadamu ni jumuiya yenye hatma ya pamoja, na watu wa magharibi hawapaswi kuchafua moyo mweupe na udhati kwa mawazo ya kisiasa, la sivyo watajuta wenyewe.