Kauli potofu za Bannon ni virusi vya kisiasa
2020-04-01 17:51:28| CRI

Hivi sasa maambukizi ya virusi vya Corona yanaenea duniani kwa haraka, na mshikamano na ushirikiano umekuwa maoni ya pamoja ya jamii ya kimataifa. Wakati huohuo, baadhi ya wanasiasa wa Marekani bado wanachochea kutengana kwa Marekani na China. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha Kauli potofu za Bannon ni virusi vya kisiasa vinavyopaswa kuondolewa.

Habari zilizotolewa na Gazeti la New York Times zinasema, Stephen K. Bannon aliyekuwa mshauri mwandamizi wa kimkakati wa Ikulu ya Marekani amesema, Marekani na China zinafanya vita za habari na uchumi, na chama tawala na serikali ya China ni tishio duniani.

alipokuwa mashauri mwandamizi wa Ikulu ya Marekani, alisema China ni adui mkuu wa Marekani. Baada ya kutokea kwa maambukizi ya virusi vya Corona, alitoa uongo kwamba China imeanzisha vita ya kivumbe.

Mtaalamu mkuu wa magonjwa ya kuambukiza wa serikali ya Marekani Anthony S. Fauci amekadiria kuwa, mamilioni ya Marekani wataambukizwa virusi vya Corona, na watu kati ya laki moja na mbili watafariki dunia. Hivyo Wamarekani wengi wenye busara wametaka kuzidisha ushirikiano na China, ili kukabiliana na virusi hivyo.

Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni alipozungumza na rais Xi Jinping wa China kwa njia ya simu aliahidi kuondoa usumbufu, ili nchi hizo mbili kushirikiana vizuri kukabiliana na COVID-19. Kauli potofu za Bannon ndio virusi vya kisiasa vinavyoleta usumbufu mkubwa na kupaswa kuondolewa.