Rais wa China asisitiza kuendeleza uchumi wa kijani
2020-04-02 17:35:10| CRI

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alipokagua kijiji cha Yucun, wilaya ya Anji mkoani Zhejiang, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza uchumi wa kijani.

Miaka 15 iliyopita, watu wa kijiji hicho walitajirika kupitia shughuli za uchimbaji wa madini na utengenezaji wa saruji, lakini shughuli hizo zilichafua mazingira ya kiikolojia ya kijiji hicho. Kuanzia mwaka 2003, kijiji hicho kilifukia mashimo ya madini na viwanda vya saruji, ili kulinda mazingira. Sasa miaka 15 imepita, kijiji hicho kimeendelea kwa kutegemea uchumi wa kijani, na mapato ya wakulima pia yameongzeka kwa kiasi kikubwa.

Hivi sasa dunia inakabiliwa na maambukizi ya virusi vya Corona, hali ambayo imeathiri vibaya uchumi wa nchi mbalimbali. Ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa wa kiuchumi, China pina inakabiliwa na changamoto kubwa. Lakini changamoto hiyo pia inahimiza China kuendeleza uchumi wa kijani. Rais Xi alipokagua mkoani Zhejiang amesema, changamoto pia ni fursa, ukishinda changamoto, itakuwa fursa.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini China Nicholas Rosellini ameipongeza China kwa kupiga hatua kubwa katika uchumi wa kijani. Wanauchumi wengi wanakadiria kuwa, katika siku za baadaye, China itatoa kipaumbele katika maendeleo ya uchumi wa kijani.