Nchi zote duniani zahimizwa kushikamana kukabiliana na COVID-19
2020-04-02 17:36:01| CRI

Wakati dunia inakabiliwa na maambukizi ya virusi vya Corona, China ambayo imefanikiwa kudhibiti virusi hivyo, inatoa misaada ya kupambana na virusi hivyo, lakini baadhi ya wanasiasa wa magharibi wanatoa kauli za kupotosha kuhusu China. Hivyo jamii ya kimataifa imehimiza nchi zote duniani zishikamane kukabiliana na COVID-19.

Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi uliopita, China imetoa misaada ya dharura kwa nchi 120 na mashirika ya kimataifa ikiwemo Shirika la Afya Duniani, Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Asia Kusini Mashariki, kutuma vikundi vya madaktari kwa nchi 7, na kufanya mikutano na nchi zaidi ya 100 kwa njia ya video ili kujulisha uzoefu wake.

Wakati huohuo, baadhi ya wanasiasa wa nchi za magharibi wameendelea kupaka matope China kwa kutoa habari na kauli mbalimbali za kupotosha, ikiwemo kwamba China imeleta virusi, China imeficha ukweli wa maambukizi ya virusi nchini humo, China ina hila ya kisiasa wakati inapotoa misaada, na vifaa vya matibabu vya China havina ubora.

Kauli hizo zimelaumiwa na jamii ya kimataifa. Mkuu wa miradi ya dharura ya Shirika la Afya Duniani WHO Michael Ryan ameonya kauli ya kulaani nchi nyingine kutotoa habari wa ukweli, kwani habari zilizotolewa na nchi mbalimbali kila siku zina ushahidi wa kutosha. Gazeti la JoongAng Ilbo la Korea ya Kusini limesema China imetoa habari wazi kwa jamii ya kimataifa toka mwanzo. Shirika la Utangazaji la Japan limesema China imetoa misaada na kutuma vikundi vya madaktari kwa nchi nyingine.

Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus amesema, virusi vya Corona ni virusi vipya, pande mbalimbali zinapaswa kuaminiana ili kukabiliana vizuri na virusi hivyo. Vita dhidi ya virusi hivyo vinahitaji juhudi za pamoja za binadamu wote.