China yaendelea kuboresha usimamizi wa jamii
2020-04-03 20:45:14| CRI

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alipofanya ukaguzi mkoani Zhejiang amesema, kutatua masuala ya jamii ni kazi ya kimsingi ya kudumisha utulivu wa taifa moja, na madhumuni ya kufanya kazi hiyo ni kuwahudumia wananchi.

Rais Xi alizungumzia kwa kina haja ya kuboresha mfumo na uwezo wa kusimamia jamii. Tangu kutokea kwa maambukizi ya virusi vya Corona, China imedumisha utaratibu mzuri wa kawaida wa jamii kwa kutegemea mfumo kamili unaoshirikisha watu wote.

Pamoja na kukabiliwa na maambukizi ya kasi ya virusi hivyo, huduma za upatikanaji wa maji, umeme, habari, chakula na vitu vingine vya lazima vya kimaisha hazikuathiriwa katika mikoa yote nchini China, ikiashiria kuwa China ina uwezo mkubwa katika usimamizi wa mambo ya kijamii.

Profesa Ravi Veriah Jacques wa Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani amesema, kushinda virusi vya Corona kumethibitisha nguvu ya mfumo wa China. Ameongeza kuwa, hakushangazwa na China kujenga hospitali ndani ya siku 10, kwani imejenga kilomita 35,000 za reli ya mwendo kasi, na kuwasaidia watu milioni mia kadhaa kuondokana na umaskini.