Je, Marekani inataka kuficha siri gani kwa kumwondolea wadhifa nahodha wa manowari ya kivita
2020-04-05 18:03:58| CRI

Baada ya kutangaza barua ya kuomba msaada wa kuwaokoa maofisa na askari kwenye manowari inayobeba ndege, Kapteni Brett Crozier aliondolewa wadhifa wake na kaimu waziri wa jeshi la majini la Marekani Bw. Thomas Modly tarehe 3 Aprili.

Chanzo cha tukio hili ni barua ya kuomba msaada. Baada ya watu wengi zaidi kwenye manowari hiyo kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona, mwishoni mwa mwezi Machi, Kapteni Crozier aliwatumia barua maofisa wa ngazi ya juu wa jeshi la majini la Marekani, akiwaeleza kuwa hali ya manowari hiyo inazidi kuwa mbaya kwa kasi, na kuomba kuondolewa haraka kwa askari elfu kadhaa kwenye manowari hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la CNN la Marekani, Kapteni Crozier aliandika kwenye barua kuwa, "Endapo sasa hazitachukuliwa hatua haraka, hawatatunza ipasavyo askari wa manowari. Lakini jambo la kuchekesha ni kwamba, jeshi la Marekani linahusisha uamuzi wa kumfukuza kazi na "uwezo mbaya wa utoaji wa uamuzi" wa Kapteni Crozier.

Maofisa wa ngazi ya juu wa Kamati ya mambo ya kijeshi ya chama cha Demokratic kwenye baraza la chini la bunge la Marekani, walipinga hatua ya kumwondolea wadhifa Kapteni Crozier, wakisema "Wakati askari na maofisa walioko kwenye Manowari ya Theodore Roosevelt wanapokabiliwa na tishio la virusi vya Corona, kuondolewa wadhifa kwa Kapteni Crozier itakuwa hatua ya kuvunja utulivu, na kuna uwezekano kuwa italeta hatari kubwa zaidi kwa watu hao."

Wachambuzi wanaona kuwa, kitendo hicho cha jeshi la Marekani kina malengo matatu, kwanza ni kumwadhibu Kapteni Crozier kutokana na kufichua siri. Tangu virusi vya Corona vilipoenea nchini Marekani, kazi ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo nchini Marekani imekuwa ikilaumiwa. Barua ya Kapteni Crozier ya kuomba msaada inaonesha hadharani hali ya ugonjwa huo kwenye Manowari na kutokuwa na udhibiti wenye ufanisi kwa jeshi la Marekani dhidi ya ugonjwa huo. Pili, jeshi la majini la Marekani linahitaji kupata mtu wa kumbebesha lawama kwa kuenea kwa virusi vya Corona kwenye manowari. Tatu, Jeshi la majini la Marekani linaona kuwa tukio hili linaathiri ushawishi wake wa kimkakati. Lengo la kuiweka manowari ya Theodore Roosevelt kwenye eneo la magharibi ya bahari ya Pasifiki ni kuweka tishio kwenye sehemu hiyo, kutangazwa kwa hali ya ugonjwa kwenye manowari hiyo kutaathiri uwezo wa mapambano wa jeshi la Marekani. Malengo hayo matatu yanalingana na wazo la serikali ya Marekani dhidi ya ugonjwa huo, ambayo inatumia nguvu kubwa katika kuficha hali halisi ya kuenea kwa ugonjwa.

Kuzingatia maslahi ya binafsi zaidi kuliko maisha kunafanya Marekani kutoweka mkazo mkubwa katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa. Tunawashauri baadhi ya maofisa wa ngazi ya juu wa mambo ya kijeshi na ya kisiasa wa Marekani, wafanye mambo halisi katika mapambano dhidi ya ugonjwa ambao unahusiana na maisha ya wananchi na askari wa Marekani.