Hivi karibuni Marekai imeahidi tena kutoa msaada wa dola milioni 225 za Kimarekani kwa nchi nyingine ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Lakini swali ni kwamba, je, ahadi hiyo itatimizwa lini?
Kabla ya hapo, mwanzoni mwa Februari waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema Marekani itatoa msaada wa dola milioni 100 za Kimarekani kwa nchi zilizokumbwa na virusi hivyo haswa China. Lakini ukweli ni kwamba, hadi sasa China bado haijapata hata senti moja kutoka Marekani. Waitalia pia hawaamini kama Marekani itawasaidia. Hoja zilizotolewa na shirika la nchi hiyo zinaonesha kuwa ni asilimia 3 tu ya Waitalia ambao wanaamini Marekani itatoa msaada.
Wakati huohuo, ikiwa nchi pekee iliyofanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona duniani, China imetoa misaada halisi kwa nchi mbalimbali duniani kadiri iwezavyo. Hadi sasa imetoa misaada kwa nchi 127 na mashirika manne ya kimataifa, na kutuma vikundi vya madaktari katika nchi 11. Licha ya hayo, pia imechangia dola milioni 20 kwa Shirika la Afya Duniani ili kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na virusi hvyo.
Wakati dunia inapokabiliwa na ugonjwa hatari ya kuambukiza, misaada ya maneno matupu ya Marekani inaonesha kuwa, nchi hiyo haijali maambukizi ya virusi, ina wasiwasi kwamba itapoteza hadhi yake ya kimataifa, na imechukulia misaada kama ni zana ya kisiasa.