Virusi vya Corona vimevumbuliwa na Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Wuhan? Ni upuuzi tu!
2020-04-21 20:30:47| CRI

Shirika la Habari la Fox la Marekani limetoa ripoti ikisema chanzo cha virusi vya Corona ni Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Wuhan, "ushahidi" wa ripoti hiyo ni maneno matupu ya "watu kadhaa wenye chanzo cha habari".

Ripoti hiyo pia iliwasiliana na mtaalamu mmoja kwa njia ya simu. Lakini licha ya kudai kwamba taasisi hiyo haina uwezo wa kutosha wa kukinga virusi, hana ushahidi halisi kuhusu madai hayo.

Wanasayansi wengi duniani wamesema, hakuna ushihidi wowote unaothibitisha kuwa virusi vya Corona vimetengenezwa katika maabara, na hadi sasa binadamu hawana uwezo wa kutengeneza virusi vya aina hiyo.

Gazeti la Science Daily la Marekani pia limesema, utafiti kwa utaratibu wa jeni ya virusi vya Corona umethibitisha kuwa vimetokea kiasili.

China inafanya uchunguzi kuhusu chanzo cha virusi hivyo, na Marekani inaweza kushirikiana na China, ili kujua chanzo cha kweli cha virusi hivyo.