Hivi karibuni baadhi ya Wamarekani walitunga na kueneza uongo kwamba "Waafrika wanabaguliwa mkoani Guangzhou, China", ili kuchochea uhasama kati ya Afrika na China.
Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama amesema, chanzo cha mgongano ni baadhi ya Wanigeira mkoani Guangdong kukataa kutii sheria ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Amevilaumu vyombo cya habari vya nchi za magharibi kwa kutengeneza video zinazohusika na tukio hilo, na kueneza habari za kupotosha kwenye mitadano ya kijamii.
Hatua kali zinazotekelezwa nchini China dhidi ya virusi vya Corona ni kwa ajli ya usalama wa raia wake na wageni wote. Ikiwa moja ya sehemu yenye shinikizo kubwa zaidi ya kuwa na kesi za maambukizi kutoka nje, mji wa Guangzhou ulifanya kampeni ya kupima watu wenye hatari zaidi, na kuweka watu elfu 15 karantini. Kati yao, 4,600 ni wageni kutoka nchi 13 zikiwemo Russia, Marekani, Austrilia na nchi za Afrika.
China imeziunga mkono nchi za Afrika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Rais Xi Jinping wa China ameongea na viongozi wa nchi nyingi za Afrika kwa njia ya simu kuhusu virusi hivyo, na pia ameihimiza jamii ya kimataifa kuongeza misaada kwa Afrika kwenye mkutano wa kundi la nchi 20. Aidha, China pia imetoa misaada mingi vya vifaa vya matibabu kwa nchi mbalimbali za Afrika. Kwa upande wa Afrika, wakati China ilipokumbwa vibaya na virusi hivyo, nchi za Afrika pia zilitoa misaada kwa wakati.
Kusaidiana kati ya China na nchi za Afrika kunathibitisha kuwa, watu wa pande hizo mbili ni ndugu, marafiki na wenzi wakubwa, uhusiano kati yao unaweza kupimwa na kuthibitishwa na historia na wakati, na hautatinganishwa na uchochezi wowote.