Ziara ya rais Xi Jinping mkoani Shaanxi yaonesha nia ya China ya kutimiza lengo la kutokomeza umaskini
2020-04-24 17:38:58| CRI

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alifanya ziara ya ukaguzi mkoani Shaanxi, na kueleza imani yake ya kutimiza lengo la kuondoa umaskini mwaka huu. Kutokana na mpango kazi, China itatokomeza umaskini uliokithiri na kumaliza ujenzi wa jamii yenye maisha bora mwaka huu.

Kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona, China bado ina nia ya kutimiza lengo hilo, na hali hii inafuatiliwa sana na jamii ya kimataifa. Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa tahariri kuhusu ziara hiyo ya rais Xi Jinping mkoani Shaanxi ambayo imeonesha nia ya China ya kutimiza lengo la kutokomeza umaskini.

Tahariri hiyo inasema, katika ziara iliyofanywa kati ya tarehe 20 na 23 mkoani Shaanxi, ambao ni moja ya mikoa yenye watu maskini zaidi nchini China, rais Xi alitoa maelekezo ya njia za kuondoa umaskini, ikiwemo maendeleo ya viwanda, ongezeko la ajira, kuimarisha afya na maendeleo ya elimu, na kutoa ishara kuwa China itatimiza lengo lake la kutokomeza umaskini uliokithiri mwaka huu. Hali hii inaonesha nia ya Chama cha Kikomunisti cha China ya kuzingatia zaidi maslahi ya watu.

Mwaka jana, mratibu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja huo nchini China Nicholas Rosellini alisema, kwa kukumbusha uzoefu wa China katika miaka 40 iliyopita tangu kutekelezwa kwa sera ya mageuzi na kufungua mlango, kuna namba moja inayoshangaza sana, kwamba China imefanikiwa kuwasaidia watu milioni 800 kuondokana na umaskini, na hayo ni mafanikio makubwa sana. Mwaka huu, kama China ikitokomeza umaskini uliokithiri kama ilivyopanga, itatimiza malengo ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa miaka 10 kabla, na hii itakuwa na maana kubwa kwa dunia.

Ziara iliyofanywa na rais Xi mkoani Shaanxi wakati wa janga la COVID-19, imetia moyo na nguvu kwa China kupambana na umaskini, na itahamasisha Wachina wote kushikamana na kutokomeza kabisa umaskini unaoikumba nchi hiyo kwa maelfu ya miaka.