Marekani kushtaki China ni kitendo cha kukwepa wajibu
2020-04-24 21:20:32| CRI

Wakati maambukizi ya virusi vya Corona yanaongezeka nchini Marekani, baadhi ya wanasiasa wa nchi hiyo wameishtaki China kwa kisingizio cha kutozuia virusi hivyo kuenea nchi za nje. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri na kusema hiki ni kitendo cha kuibebesha China wajibu.

Tahariri hiyo inasema badala ya kufuatilia usalama wa maisha ya watu, wanasiasa wengi wa Marekani wamezingatia zaidi maslahi yao ya kisiasa, na wamechelewa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona na kuleta athari mbaya. Sasa wanataka China iwajibike badala yao. Watu wanaopaswa kushtakiwa ndio wanasiasa hao.

Tahariri hiyo inasema shtaka hilo halina msingi wowote wa kisheria. Kutokana na kanuni ya kusamehewa kwa nchi yenye mamlaka, mahakama ya nchi yoyote haina haki ya kushtaki serikali ya nchi nyingine.

Hadi sasa kesi za maambukizi ya virusi vya Corona zimezidi laki 8.6 nchini Marekani, na wanasiasa wa Marekani wanatakiwa kuacha siasa na badala yake kujishughulisha na juhudi za kuokoa maisha ya Wamarekani.