China yatoa kipaumbele kwa wananchi wakati wa mapambano dhidi ya COVID-19
2020-04-26 18:12:18| CRI

Tokea idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona iongezeke kwa zaidi ya elfu 13 kwa siku, hadi kufikia leo tarehe 26 wagonjwa waliotibiwa hospitali mjini Wuhan wote wamepata nafuu, imeonesha ushindi katika vita vya kulinda mji wa Wuhan, vilevile inamaanisha kuwa baada ya juhudi kubwa, wananchi wa China wamepata mafanikio makubwa katika kuzuia na kudhibiti virusi vya Corona kwa ushirikiano.

Wataalamu wengi wamekuwa wakitafiti, kwa nini China imeweza kukabiliana kwa njia zenye ufanisi tukio hili kubwa la dharura la afya ya umma ambalo limeenea kwa kasi zaidi na kwenye eneo kubwa zaidi, na ni vigumu kudhibitiwa? Kwa kweli, jibu ni rahisi: mambo yote yanafanyika kwa ajili ya wananchi na kwa kutegemea wananchi.

Hakuna vyama vingi vilivyofanya kama Chama cha Kikomunisti cha China kuuhusisha utoaji kwa wananchi kwenye kanuni za chama, na kutekeleza madaraka kwa kufuata wazo la kujiendeleza kwa kuwatilia maanani wananchi. Baada ya janga hili kutokea, rais Xi Jinping amekuwa akisisitiza kutoa kipaumbele kwa usalama na afya ya wananchi, na kuwahamasisha watu kote nchini kuwaokoa wagonjwa kadiri iwezekanavyo ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi.

Mji wa Wuhan mkoani Hubei ilikuwa sehemu iliyoripoti mapema zaidi kuwa na maambukizi ya virusi hivyo nchini China, pia ilikuwa sehemu iliyoathiriwa vibaya zaidi nchini China. Rais Xi aliweka uamuzi sahihi kwa kufuata hali ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo, na kwenda mjini Wuhan kuongoza kazi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi. China ilichukua hatua madhubuti, zenye unyumbuvu na zenye ufanisi zaidi za kuzuia na kudhibiti maambukizi katika historia.

Tarehe 23 Januari mji wa Wuhan wenye idadi ya watu zaidi ya milioni 11 ulifunga kwa muda njia za kwenda nje. Hatua hiyo kali zaidi ya kuweka karantini imekuwa na umuhimu mkubwa katika kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Gazeti la Sayansi lililotolewa tarehe 6 Machi limedhihirisha kuwa, hatua hiyo ya China ilichelewesha siku 3 hadi 5 kuenea kwa maambukizi ya virusi nchini China, na kupunguza kwa asilimia 80 kusambaa kwa ugonjwa huo duniani hadi kufikia katikati ya mwezi Februari.

Ndani ya siku kadhaa, mji wa Wuhan ulijenga hospitali mbili maalumu za kiwango cha juu, na hospitali nyingi za muda kwa wagonjwa wenye hali nzuri. Asilimia 1 ya vitu vya matibabu kwa wagonjwa mahututi vilisafirishwa kwa kasi kwenda Wuhan, na wahudumu wa afya zaidi ya elfu 40 kutoka sehemu mbalimbali walikwenda kutoa msaada mjini humo. Wakati huo huo sehemu mbalimbali za China zilichukua hatua kali kugundua wagonjwa wapya, kufuatilia watu wenye mawasiliano ya karibu na wagonjwa, na kutekeleza hatua za kuweka karantini za kukaa nyumbani, ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Tarehe 24 Aprili, wagonjwa wote mahututi wa virusi vya Corona walipata nafuu. Jambo linalofuatiliwa ni kuwa, asilimia 70 kati ya wagonjwa zaidi ya 2,500 wenye umri zaidi ya miaka 80 mjini Wuhan walipona, na mgonjwa mwenye umri mkubwa zaidi ni miaka 108. Iwe wazee au watoto, ama matajiri au maskini, usalama wa maisha ya watu wote unazingatiwa nchini China. Kama mshauri mwandamizi wa katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Bruce Aylward alivyosema baada ya kufanya ukaguzi kuhusu hali ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo nchini China, "Kutumia kila kinachowezekana, na kuokoa maisha ya watu wote kadiri iwezavyo. Mbinu zilizotumiwa na China zimethibitishwa kuwa ni sahihi."

Profesa Bw. Zheng Yongnian wa Chuo Kikuu cha Singapore ameeleza kuwa, siku zote kutoa kipaumbele kwa usalama na afya ya wananchi ni kanuni kuu ya China kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Mwanataaluma wa Akademia ya sayansi ya kijamii ya Uingereza Bw. Martin Albrow, amesema jambo linalofuatiliwa na watu ni kuwa, mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona ya China yameonesha ushirikiano, bidii, na kujizuia kwa wachina, utulivu moyoni na maadili mazuri wakati wa kukabiliana na janga hili.

Mafanikio yanategemea mshikamano na ushirikiano. Hivi sasa China inafanya juhudi kubwa za kufufua uchumi, na ina imani na uwezo wa kutimiza lengo la kujenga kwa pande zote jamii yenye maisha bora kwa mwaka huu. "Mambo yote yanafanyika kwa ajili ya wananchi, na pia yanategemea wananchi" na huu ni msukumo mkubwa kwa China kupiga hatua ya kutimiza malengo yake.