Mfumo wa kisiasa umechangia mfanikio ya China katika kudhibiti virusi vya Corona
2020-04-27 17:58:35| CRI

Wakati nchi mbalimbali zinajitahidi kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, China imepata mafanikio muhimu katika kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo, ambavyo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amevielezea kuwa ni utatanishi mkubwa zaidi duniani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Akieleza maoni yake juu ya mafanikio hayo, mwenyekiti wa Mfuko wa The Kuhn wa Marekani Bw. Robert Lawrance Kuhn amesema, ni kutokana na uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, mfumo wa kisiasa wa China na serikali yenye nguvu, China imeweza kukabiliana na ugonjwa huo kwa nguvu, ufanisi na kwa haraka.

Kama alivyosema Bw. Kuhn, wasomi na wachambuzi wengi wanasema uongozi imara wa CPC ni sababu muhimu ya kuifanya China ipate ushindi muhimu katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona ndani ya muda mfupi, na pia umeonesha sifa bora ya mfumo wake wa kisiasa ikiwemo uwezo mkubwa wa kuhamasisha na "kukusanya nguvu kufanya jambo kubwa".

Kutokewa na janga kama hilo likiloibuka ghafla, karibu nchi zote zinakabiliwa na changamoto kama vile upungufu wa wahudumu wa afya, uhaba wa vitanda katika hospitali na vifaa vya matibabu. Lakini kutokana na uwezo mkubwa wa kuhamasisha na kuongoza jamii, China ilitatua changamoto hizo.

Inafahamika kuwa ili kusaidia mkoa wa Hubei na mji wa Wuhan kukabiliana na virusi hivyo, China ilipeleka vikosi zaidi ya 330 vya matibabu na wafanyakazi elfu 42 wa afya kutoa msaada katika mji na mkoa huo. Ili kuhakikisha kila mgonjwa anatibiwa, Wuhan ilijenga hospitali maalum na hospitali za muda za kuwatibu wagonjwa wa virusi vya Corona. Viwanda vilijitahidi kuanzisha shughuli zao na kutengeneza barakoa na nguo za kujikinga na virusi na kuzipelekea kwa wahudumu wa afya waliokuwa mstari wa mbele. Ni wazi kuwa, kuyapa kipaumbele maisha ya watu ni msingi wa kazi ya kuzuia na kudhibiti virusi nchini China, na kwamba gharama zote za matibabu ya wagonjwa zinalipwa na bima na serikali.

Baada ya maambukizi kudhibitiwa, China iliamua kuongeza kasi ya kurudisha utaratibu wa kijamii na kiuchumi, na alipofanya ziara ya ukaguzi mkoani Zhejiang mwezi Machi, rais Xi Jinping wa China alisema "ni uwezo wa nchi kutekeleza maagizo mara moja na kuacha jamii irudi kwenye utaratibu wa kawaida baadaye "

Hata hivyo, kitu chochote duniani kina mapungufu yake. Ikikabiliwa na tishio la janga hilo, ama kwa nchi za magharibi, au kwa nchi zinazoendelea, zote zimeonesha mapungufu na matatizo yao. Viongozi wa China wamebainisha kuwa, China inatakiwa kujifunza kutokana na tukio hilo, kwani kukabili tatizo moja kwa moja na kuwa na ujasiri wa kujirekebisha pia ni sifa bora ya mfumo wa kisisa wa China.

"Historia huwa inapiga hatua kubwa mbele baada ya kukumbwa janga." Baada ya kupitia mtihani huu, mfumo wa kisiasa wa China na uwezo wake wa usimamizi unatarajiwa kukamilishwa zaidi, na China itakuwa na nia imara zaidi ya kupambana na changamoto mbalimbali katika njia ya kusonga mbele.