Mlipuko wa virusi vya Corona ulianza ghafla bila kutarajiwa nchini China mwanzoni mwa mwaka 2020, lakini kutokana na uongozi wa rais Xi Jinping wa China, wachina bilioni 1.4 wameshikamana na kusaidiana, na kupata mafanikio muhimu katika kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo mjini Wuhan na nchini China kwa ujumla.
Tangu kutokea kwa mlipuko huo, rais Xi aliongea kwa njia ya simu na viongozi wa nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa, na alisisitiza kuwa "binadamu ni jumuiya yenye hatma ya pamoja" na "mshikamano na ushirikiano ni silaha zenye nguvu zaidi". Kwenye mkutano maalum wa kilele wa wakuu wa kundi la G20 uliofanyika tarehe 26, Machi, rais Xi alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kujizatiti kwa imani, kushikamana na kukabiliana na virusi vya Corona kwa ushirikiano. Pia alitoa mapendekezo manne: kufanya vizuri vita vya kupambana na virusi vya Corona duniani, kushirikiana kimataifa katika kuzuia na kudhibiti virusi vya Corona, kuunga mkono mashirika ya kimataifa kuonesha umuhimu wake, na kuimarisha uratibu wa sera za kiuchumi duniani.
Wakati huohuo, China imekuwa ikifuata kanuni ya uwazi na uwajibikaji, na kutoa taarifa kwa wakati kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusiana na maambukizi ya virusi vya Corona, kueleza mapema utaratibu wa vinasaba vya virusi hivyo, na kufanya ushirikiano wa kimataifa kati ya wataalam kuhusu kuzuia na kudhibiti maambukizi hayo. Mpaka mwisho wa mwezi Machi, virusi vya Corona vilienea kwa kasi kwenye nchi na sehemu zaidi ya 200 duniani, na kutoa changamoto isiyo na mfano kwa usalama wa afya ya umma duniani. China, mbali na kufanya vizuri kazi zake za kuzuia kuenea kwa virusi ndani ya nchi, imetoa msaada kwa dunia kadri ya uwezo wake, ikiwemo kuchangia vifaa vya matibabu na kueleza uzoefu wake katika kuzuia kuenea kwa virusi na kutibu wagonjwa.
China kufanya hivyo sio tu ni kushukuru uungaji mkono na misaada iliyotolewa na jamii ya kimataifa wakati ilipokabiliwa na maambukizi ya kasi ya virusi vya Corona, pia ni msaada unaotolewa kwa maisha ya watu katika msingi wa moyo wa ubinadamu. Vilevile ni vitendo halisi vya kutekeleza wazo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja lililotolewa na rais Xi, na kwamba katika wakati huu, China ina wajibu wa kulinda usalama wa afya ya umma duniani na maendeleo ya binadamu.
Virusi havijali mipaka ya nchi, na vinaweza kumwambukiza mtu yeyote. Kushikamana, kushirikiana, kusaidiana na kukabiliana kwa pamoja na virusi ndio matumaini kwa binadamu kushinda janga hili linalowakabili binadamu wote. Kama alivyosema waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger katika makala yake ya "janga la virusi vya Corona litabadili utaratibu wa dunia daima", kuwa hakuna nchi yoyote inaweza kushinda virusi kwa kutegemea nguvu yake binafsi, na ufumbuzi wa kutatua tatizo la sasa unatakiwa kuunganishwa na dira na mpango wa ushirikiano wa kimataifa.