Mshauri mwandamizi wa Katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Bruce Alyward baada ya kumaliza ziara yake nchini China mwishoni mwa mwezi Februari, alisema kuwa watu wa China wameonesha nguvu kubwa inayotokana na ushirikiano na mwitikio wa pamoja.
Ofisa huyo anaona kuwa, nguvu hiyo inayoiwezesha China kupata ushindi kwa haraka kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona, ni matokeo ya mkakati sahihi wa kuzingatia maslahi ya watu uliowekwa na rais Xi Jinping wa China, ambaye aliongoza mwenyewe vita hiyo dhidi ya virusi. Na mtizamo wa kujali maslahi ya watu ndio ni sehemu ya msingi wa utamaduni wa taifa la China.
Ustaarabu wa China ukiwa ni ustaarabu wa tangu kale ambao haukuwahi kukatika kwenye historia ya binadamu, maadili yake bora yameonekana wazi katika juhudi za kudhibiti mlipuko huu wa virusi vya Corona. Kila mchina anapokabiliwa na changamoto, maslahi yake binafsi huwa yanaitikia maslahi ya umma, na wananchi wote wanasaidiana na kuungana mikono mbele ya janga hilo, na hivyo vyote ndivyo ni matokeo ya urithi wa utamaduni bora wa taifa la China yenye historia ya miaka elfu tano.
Inaonekana wazi kuwa utamaduni wa China umeonesha nguvu yake kubwa katika kukabiliana na janga hilo la virusi vya Corona. Katika miezi mitatu iliyopita tangu mlipuko wa virusi hivyo ulipoibuka, jumuiya ya kimataifa imeona kuwa manufaa ya kimfumo ni silaha muhimu kwa China kushinda vita hiyo dhidi ya virusi, na kutumia vizuri manufaa hayo ya kimfumo na kitaasisi, hakuondokani na urithi wa utamaduni wa taifa la China.
Wakati wa kukabiliana na janga hilo, kulinda na kuokoa maisha ya wananchi siku zote ni kipaumbele kwa Chama tawala cha China, kama ilivyosisitizwa mara nyingi na Rais Xi Jinping. Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai hivi karibu pia amesema kuwa kuzingatia afya ya wananchi ni jambo muhimu kabisa kwa China, haswa kuwalinda wazee, watu wenye magonjwa sugu na watu maskini. Amesema, Chama tawala cha China siku zote kinashikilia moyo wa kuwahudumia wananchi, na hivyo kuungwa mkono na kuaminiwa na wananchi wa China.
Wachambuzi wanaona kuwa, uzalando na moyo wa kujitolea wa watu wa China pia vimetoa mchango mkubwa katika kuiwezesha China kushinda mapambano dhidi ya janga hilo. Takwimu zinaonesha kuwa tangu janga hilo litokee, madaktari elfu 42 kutoka sehemu mbalimbali za China walijitolea kwenda Wuhan, na watu bilioni 1.4 wa China walitikia kwa pamoja wito uliotolewa na serikali wa kukaa nyumbani, ikiwa ni mchango mdogo wa kila mwananchi kwa juhudi kubwa za kitaifa.
Falsafa ya Wachina inaona kuwa majanga hustawisha taifa. Janga hilo la virusi vya Corona ni kama wimbi lingine tena kwa taifa la China kwenye mchakato wake wa kutimiza ustawi mpya, ambapo watu wa China wameonesha mara nyingine tena nguvu kubwa ya kuweza kushinda taabu na changamoto.