Sekta ya utalii stawi yaonesha kufufuka kwa uchumi wa China
2020-05-06 17:15:13| CRI

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zinaonesha kuwa, katika siku tano za mapumziko ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Wachina zaidi ya milioni 115 walifanya utalii. Hali hii inaonesha kuwa athari ya mlipuko wa virusi vya Corona ni ya muda mfupi, na uchumi wa China unafufuka kwa haraka.

Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, pato la utalii katika siku hizo tano nchini China lilifikia karibu dola bilioni 6.7 za kimarekani. Ingawa kiasi hicho ilikuwa asilimia 40 ya mwaka jana kipindi kama hiki, lakini kimepatikana wakati China bado haijafungua kabisa shughuli za utalii kufuatia maambukizi ya virusi vya Corona. Hali hii inaonesha kuwa sekta ya utalii ambayo ni moja ya sekta zinazoathiriwa zaidi na virusi hivyo inafufuka nchini China.

Wakati huohuo, matumizi ya watu wa China pia yanaongezeka. Katika siku hizo za mapumziko, mauzo ya maduka mengi makubwa mjini Wuhan yalirejea kwenye kiwango cha wakati kabla ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona. Mji wa Shanghai uliandaa sikukuu ya ununuzi ya tarehe 5, Mei, na mauzo ya bidhaa ndani ya saa 18 yalizidi dola bilioni 1.4 za Kimarekani.

Matumizi yamekuwa injini kuu ya ukuaji wa uchumi wa China kwa miaka mingi. Ongezeko la matumizi katika siku za mapumziko ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani limeonesha kufufuka kwa uchumi wa China.

Hivi sasa, China inaendelea kuharakisha kurejesha uzalishaji, na katika mwezi Machi na Aprili, kiashiria cha manunuzi kwa sekta za uzalishaji PMI kilikuwa juu ya asilimia 50, ambayo ni kipimo cha kudidimia au kufufuka kwa uchumi.

Ikiwa nchi iliyochangia ongezeko la uchumi wa dunia kwa asilimia 30 katika miaka mingi iliyopita, China kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona na kuharakisha kurejea kwa uzalishaji kumetia moyo kwa uchumi wa dunia. Gazeti la Financial Times la Uingereza limesema, moja ya sababu za kufufuka kwa soko la hisa la Marekani ni matarajio kwamba China itaongoza dunia kufufua uchumi.

Wachina wanaamini kuwa, msukosuko huambatana na fursa. Ukikabiliwa na maambukizi ya virusi vya Corona, uchumi wa China si kama tu umeonesha nguvu kubwa ya kufufuka, bali pia umepata injini nyingi mpya, hali inayothibitisha kuwa mwelekeo mzuri wa uchumi wa China haubadiliki. Hivi sasa hali ya maambukizi ya virusi vya Corona bado inatatanisha, na hakuna nchi yoyote inayoweza kujitenga na hali hiyo. Ushirikiano wa kimataifa unahitajika katika kukabiliana na virusi hivyo na kufufua uchumi.