Mashambulizi yanayofanywa na baadhi ya wanasiasa wa Marekani yatawaharibia wenyewe
2020-05-07 19:23:01| CRI

Wakati hali ya maambukizi ya virusi vya Corona ikionesha mwelekeo mzuri huku maisha ya kawaida ya watu yakirejea hatua kwa hatua katika nchi nyingi duniani, Marekani ikiwa nchi pekee inayoongoza duniani inadumisha ongezeko la idadi ya watu walioambukizwa zaidi ya elfu 20 kwa siku, hali ambayo inasikitisha watu.

Baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanapuuza watu walio hatarini na kujitafutia maslahi ya kisiasa kwa kusambaza uvumi mbalimbali, kama ule unaodai kuwa "Chanzo cha virusi kilitoka kwenye maabara ya mji wa Wuhan wa China" na pia "Kukataza uhusiano wa kiuchumi na China" ambao si kama tu unakwenda kinyume cha kanuni za kisayansi, pia haulingani na kanuni za kiuchumi, na utaathiri maisha ya wananchi na kudhuru maendeleo ya uchumi wa Marekani, ambayo yamekuwa "mashambulizi ya kujiharibia".

Hadi sasa utafiti wa wanasanyansi wa nchi nyingi umethibitisha kuwa virusi vya Corona havikutengenezwa kwenye maabara. Lakini baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanafumba macho na masikio yao, wakishikilia kuwa wana ushahidi unaothibitisha kuwa virusi hivyo vilitoka kwenye maabara ya Wuhan. Aliyekuwa mshauri mkuu wa Idara ya upelelezi ya Marekani FBI Bw. Andrew Weissmann anaona kuwa kauli hiyo inaweza kuorodheshwa kati ya "Habari feki za Ikulu ya Marekani", na inawashangaza watu kama kiongozi wa Marekani alivyosema kuwachoma watu sindano zenye dawa za kuulia wadudu kunaweza kuua virusi vya Corona.

Jambo lingine ni kuwa, jumatano wiki hii, ofisa wa serikali ya Marekani alipojibu maswali ya waandishi wa habari alisema, Marekani haina uhakika kuwa virusi vya Corona vinatoka kwenye maabara ya mji wa Wuhan, huku akijitetea kuwa kauli hiyo haigongani na ile ya awali ambapo alisema "kuna ushahidi mkubwa unaothibitisha kuwa virusi hivyo vilitoka kwenye maabara ya Wuhan". Kitendo hicho kimewashangaza sana watu.

Hivi sasa kuna ushahidi mwingi unaothibitisha kuwa, watu walioambukizwa virusi vya Corona walionekana nchini Marekani mapema zaidi kuliko ilivyotangazwa na serikali yake, na kuna uwezekano kuwa virusi hivyo vilienea kwenye mitaa ya Marekani wakati wa maambukizi ya mafua yalipotokea mwezi Septemba mwaka jana nchini humo.

Mbali na kueneza uvumi mbalimbali, baadhi ya wanasiasa hao pia wanajaribu kuhamasisha makampuni ya Marekani kuondoka kutoka China, ili kutimiza kukataza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani. Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na Shirika la habari la Uingereza Reuters, serikali ya Marekani inaharakisha mpango wa kuitoa China kutoka kwenye minyororo wa viwanda na utoaji wa bidhaa duniani. Lakini ukweli umeonesha kuwa, makampuni mengi ya Marekani yanaongeza uwekezaji nchini China, kwa mfano kampuni ya Starbucks imesaini mkataba na mji wa Kunshan, mkoani Jiangsu, kujenga Eneo la uvumbuzi la viwanda la mgahawa, Kampuni ya Tesla imetangaza kuongeza uwezo wa uzalishaji kwenye kiwango chake mjini Shanghai, na Mradi wa madini ya Ethylene unaowekezwa dola za kimarekani zaidi ya bilioni 10 na Kampuni ya Exxon Mobil umezinduliwa rasmi mjini Huizhou. Makampuni hayo ya Marekani yameonesha imani yao juu ya soko na uchumi wa China.

Wanasiasa wa Marekani wanajitahidi sana licha ya ukweli wa mambo kuwa wazi. Marekani inapoteza si tu maisha ya watu, bali pia ni kuvunjika kwa heshima ya nchi kutokana na mashambulizi ya kujiua yanayofanywa na wanasiasa wao.