Wanasiasa wa Marekani wanawachukua wananchi kama chombo cha kufanyiwa majaribio
2020-05-08 21:18:04| CRI

Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya utafiti na maendeleo ya matibabu ya kiikolojia ya Marekani Bw. Rick Bright ameilaani serikali ya Marekani kwa kulazimishwa kutii amri mbele ya mambo ya kisiasa na kuacha kufuata mapendekezo ya wataalamu hodari wa sayansi kwenye serikali wakati inapotoa maamuzi kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Katika ripoti ya kurasa 86 aliyoitoa kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka wa nchi hiyo, Bw. Bright alifafanua jinsi serikali ya Marekani ilivyoshindwa kuchukua hatua zenye ufanisi katika mapambano dhidi ya virusi hivyo, na kuilaani kwa kufukuzwa kazi kwa kukiuka kanuni zinazohusika, hali ambayo imewafanya watu watambue wazi kuwa ni watu wanaotumia madaraka yao vibaya na kutoa maamuzi yasiyofaa ndio wamesababisha kushindwa kwa kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.

Watoaji wa maamuzi wa serikali hawatoi kipaumbele kwa mapambano dhidi ya ugonjwa huo, badala yake wanafikiria zaidi maslahi yao binafsi, nkuwachukulia wananchi wake kama chombo cha kufanyiwa majaribio, na kukosa wakati muhimu wa kuzuia ugonjwa huo.

Aidha mamlaka ya utawala ya Marekani haikuchukua njia ya kisayansi wakati wa kutoa maamuzi. Ripoti aliyoitoa Bw. Bright inasema, baada ya mlipuko wa janga la COVID-19 kutokea nchini Marekani, alikosana na wafuasi wa kiongozi wa Marekani kwenye wizara za afya na utoaji wa huduma ya umma kutokana na kukataa kueneza dawa ambalo halijathibitishwa kwa njia ya kisayansi, na kuondolewa kwenye wadhifa wake.

Marekani ikiwa nchi inayoongoza kwa kumiliki matibabu ya kisasa duniani, inatakiwa kufikiria kwa makini kwa nini hasa imeshindwa kuzuia maambukizi ya virusi, na imeshindwa kuokoa maisha ya wananchi wake kwa njia ya kuwakosoa wengine. Kuweka kando maslahi binafsi na kutilia mkazo katika kuzuia maambukizi ya virusi ni njia pekee ya kujiokoa.