Marekani yachukulia mapambano dhidi ya COVID-19 kama ni michezo ya kisiasa
2020-05-09 20:58:12| CRI

Gazeti la The Sydney Morning Herald la Australia limetoa ripoti likisema, waraka wenye kurasa 15 uliotolewa tarehe 2 na Gazeti la The Daily Telegraph na kudai chanzo cha virusi vya Corona ni Maabara ya Utafiti wa Virusi ya Wuhan, China, unatokana na habari mbalimbali zisizo sahihi, na kuaminiwa kuwa umetolewa na mwanadiplomasia wa Marekani nchini Australia. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri, na kusema Marekani inachukulia mapambano dhidi ya COVID-19 kama ni michezo ya kisiasa.

Tahariri hiyo inasema, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alikiri kuwa Marekani ni mwongo, tapeli, na mwizi katika mambo ya kimataifa. Baada ya kutokea kwa mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona, Marekani imefanya hivyo tena, na kuwafahamisha watu wote duniani ukweli wa "fahari Marekani inayoendelea kujipatia".

Tangu kutokea kwa COVID-19, baadhi ya wanasiasa wa Marekani wametunga uwongo kuipaka matope China kadiri wawezavyo. Makala iliyotolewa na Gazeti la Foreign Policy la Marekani inasema, sababu yao ya kufanya hivyo ni uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba nchini humo, wanataka kuelekeza makosa kwengine kwa kutokabiliana vizuri na ugonjwa huo, ili kuepuka kushindwa kwenye uchaguzi huo. Marekani imechukulia mapambano dhidi ya COVID-19 kama ni michezo ya kisiasa.