Viongozi wa Marekani wapaswa kuwajibika na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona duniani
2020-05-13 20:04:14| CRI

Hivi karibuni, msomi maarufu wa Marekani Bw. Noam Chomsky ameilaani serikali ya nchi hiyo akieleza kuwa ili kuficha makosa waliyoyafanya kwa Wamarekani, viongozi wa Marekani wametafuta njia ya kuhamisha uwajibikaji wao.

Kabla ya kulipuka kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo, wataalamu kutoka Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani, Shirika la Afya Duniani WHO na China walitoa onyo mara nyingi, lakini viongozi wa Marekani walipuuza onyo hilo. Wakati maambukizi hayo yalipoonesha mwelekeo wa kushindwa kudhibitiwa, hawakuchukua hatua yoyote yenye ufanisi, badala yake waligeuza mlipuko huo kuwa suala la kisiasa na kuhamisha uwajibikaji wake kwa wengine.

Kwa kushindwa kuzuia maambukizi hayo, Marekani imekuwa sehemu dhaifu zaidi duniani, na pia kuwa nchi inayoongoza kwa kueneza idadi kubwa ya watu wenye maambukizi duniani.

Jamii ya kimataifa ina wasiwasi mkubwa na hatua za Marekani katika kuzuia na kudhibiti janga hili, bado haijajulikana idadi ya watu watakaofariki kutokana na makosa ya viongozi wa Marekani.