Zaidi ya viongozi 140 wa nchi mbalimbali wakiwemo rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, waziri mkuu wa Pakistan Bw. Imran Khan na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown wameandika barua ya pamoja, wakitaka nchi zote zipate chanjo dhidi ya virusi vya Corona kwa usawa, kama ikitafitiwa na kutengenezwa kwa mafanikio.
Barua hiyo imetolewa baada ya Kampuni kubwa ya Dawa ya Sanofi ya Ufaransa kusema chanjo hiyo ikiwa tayari, itatolewa kwa Marekani kwanza. Kabla ya hapo, serikali ya Marekani ilijaribu kununua teknolojia ya chanjo ya COVID-19 ya kampuni moja ya Ujerumani, ili kuitumia peke yake. Kwenye mkutano wa kimataifa wa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, nchi nyingine zimeichanga Euro bilioni 7.4 kwa ajili ya utafiti, kutengeneza na kugawanya kwa usawa kwa chanjo ya virusi hivyo, isipokuwa kwa Marekani ambayo haikutoa hata senti moja.
Licha ya hayo Marekani ilitunga uwongo kwamba, China inajaribu kuiba teknolojia ya chanjo hiyo kutoka kwa Marekani. Lakini ukweli ni kwamba China imekuwa mbele zaidi katika utafiti wa chanjo hiyo.
Tangu kutokea kwa maambukizi ya virusi vya Corona, Marekani imefanya mambo mengi mabaya, yakiwemo kuchukua vifaa vya kukabiliana na virusi vya nchi nyingine, kukataa kulipa ada kwa Shirika la Afya Duniani, na kufanya umwamba katika utafiti wa chanjo. Kutokana na vitendo hivyo, Marekani imekuwa kizuizi kwenye ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na COVID-19. Mhariri mkuu wa Jarida la The Lancet la Uingereza Bw. Richard Horton, amesema Marekani inafanya uhalifu na usaliti dhidi ya binadamu wote.