Wanasiasa wa Marekani wafanya ubaguzi wa rangi wakati wa janga la COVID-19
2020-05-18 20:07:35| CRI

Tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona nchini Marekani, ili kukwepa wajibu wa kutokabiliana vizuri maambukizi ya virusi hivyo, wanasiasa wa nchi hiyo wamechochea uhasama kati ya watu wa makabila tofauti, na kufanya ubaguzi wa rangi.

Mara nyingi Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameviita virusi vya Corona ni "Virusi vya Wuhan", hata kwenye majukwaa ya kimataifa. Ofisa mwandamizi mwingine wa nchi hiyo Peter Navarro hivi karibuni alitoa kauli isiyo na ukweli kwamba, China ilituma malaki ya watu "kupandikiza" virusi katika sehemu mbalimbali duniani.

Kutokana na uchochezi wao, vitendo vya ubaguzi nchini Marekani vimepamba moto. Habari zilizotolewa na tovuti ya Jarida la The Times la Marekani zinasema, tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona, jarida hilo limeshuhudia kesi zaidi ya 1,200 za ubaguzi dhidi ya Waasia.

Ubaguzi umedumu kwa muda mrefu nchini Marekani, na imekuwa maradhi sugu kwa mfumo wa utawala wa nchi hiyo. Hojaji iliyofanywa na Gazeti la The Washington Post inaonesha kuwa, kutokana na virusi vya Corona, kiwango cha ukosefu wa ajira kwa watu wa asili ya Latin-Amerika na Waafrika nchini Marekani kimefikia asilimia 20 na 16, huku kiwango hicho ni asilimia 11 kwa Wazungu. Licha ya hayo, mwanasayansi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Afya ya Marekani Kizzmekia Corbett amesema, Waafrika hawapati huduma zinazostahili ikiwa hospitali inakosa vifaa vya kutosha vya kupumua.

Gazeti la The Washington Post limenukuu Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani likisema, Waafrika na watu wa wengine wenye rangi wameathiriwa zaidi na virusi vya Corona. Takwimu zilizotolewa katikati ya mwezi April na Mfuko wa Ugonjwa wa UKIMWI wa Marekani pamoja na na Chuo Kikuu cha Emory cha nchi hiyo zinaonesha kuwa, Waafrika wanaochukua asilimia 13 ya idadi ya watu ya Marekani wameshika asilimia 52 ya wagonjwa wa COVID-19, na asilimia 58 ya vifo kutokana na ugonjwa huo.

Badala ya maisha ya watu, wanasiasa wa Marekani wanazingatia zaidi maslahi yao ya kisiasa, na wanasukuma nchi yao kwenye njia ya giza na uhasama. Lakini watu wanaochochea ubaguzi hakika wataumia wenyewe.