Baadhi ya wanasiasa wa Marekani hawatafanikiwa katika suala la Taiwan kujiunga na mkutano wa afya wa dunia
2020-05-19 20:58:45| CRI

Mkutano wa 73 wa Afya wa Dunia unafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 22 mwezi huu kwa njia ya video, na kama ilivyotarajiwa, Taiwan ilikataliwa tena kuhudhuria mkutano huo. Hali hii inathibitisha tena kuwa, jamii ya kimataifa imekataa wanasiasa wa Marekani kuvurugu mkutano huo katika suala la Taiwan.

Kuanzia mwezi huu, ili kuhamisha ufuatiliaji kwa makosa yake ya kutokabiliana vizuri maambukizi ya virusi vya Corona, na kutaka kuiwajibisha China, Marekani iliongeza sauti ya kuiunga mkono Taiwan kujiunga na Mkutano wa Afya wa Dunia. Kwa mfano, wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imetoa makala nyingi kuunga mkono Taiwan kwenye Twitter, wenyeviti wa kamati za mambo ya nje za mabaraza mawili ya bunge la nchi hiyo waliandikia barua kwa serikali za nchi karibu 60, na kuzitaka kuunga mkono Taiwan, na baraza la seneta la bunge hilo lilipitisha mswada wa kumtaka waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kuandaa mpango wa kuisaidia Taiwan kupata kiti cha uangalizi katika Shirika la Afya Duniani WHO.

Hata hivyo, wanasiasa hao wanafahamu vizuri kuwa, mbele ya kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani, majaribio yote yanayohusisha suala la Taiwan yatashindwa, kwani Jamhuri ya Watu wa China ni mwanachama pekee halali katika mfumo wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na WHO. Lengo la kucheza michezo ya kisiasa kuhusu Taiwan si kulinda maslahi yake, bali ni kuzuia maendeleo ya China.

Ukweli ni kwamba, kwa kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani, serikali kuu ya China ina mpango kamili kuhusu Taiwan kujiunga na mambo ya kiafya duniani. Tangu mwaka jana, vikundi 16 vya wataalamu wa afya wa Taiwan wameshiriki kwenye shughuli za WHO. Baada ya kutokea kwa mlipuko wa COVID-19, serikali kuu ya China iliwaalika wataalamu wa Taiwan kufanya ukaguzi mjini Wuhan ili kufahamu mlipuko huo. Hadi tarehe 15 mwezi huu, China bara imetoa habari kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona kwa Taiwan kwa mara 152.

Tahariri iliyotolewa na Gazeti la the Rhine Post la Ujerumani inasema, Marekani haina maslahi katika Taiwan, inaichukua Taiwan kama ni fursa ya kuhamisha ufuatiliaji kwa serikali ya Marekani kutokabiliana vizuri na virusi vya Corona. Wakati uchaguzi mkuu unapokaribia, wanasiasa wa Marekani wameibua tena suala la Taiwan.

Hadi sasa vifo vya watu kutokana na COVID-19 vimezidi elfu 90. Watalaamu wameonya kuwa hali ya maambukizi itakuwa mbaya zaidi katika siku zijazo. Wanasiasa wa Marekani wanatakiwa kuzingatia zaidi juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo. Kwani, ukweli umethibitisha kuwa kucheza kadi ya Taiwan haiwezi kutishia China, na pia hakukubaliwi na jumuiaya ya kimataifa.