Uchumi wa China wafufuka baada ya mlipuko wa COVID-19
2020-05-20 18:59:18| CRI

Mikutano Mikuu Miwili ya kisiasa nchini China itafanyika kuanzia kesho, wakati dunia inakabiliwa na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona na kudidimia kwa uchumi, jamii ya kimataifa inafuatilia sana jinsi China itakavyohimiza maendeleo ya uchumi wakati wa kukabiliana na virusi hivyo. Shirka Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri, ikisema China ina imani na uwezo wa kushinda changamoto, na kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii.

Tahariri hiyo inasema viashiria mbalimbali vya kiuchumi vilivyotolewa hivi karibuni vinaonesha kuwa, uchumi wa China unafufuka kwa haraka. Kwa mfano, ongezeko la thamani ya uzalishaji wa kiviwanda kwa mwezi April liliongezeka kwa asilimia 3.9 ililinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho, huku mauzo ya bidhaa za China kwa nchi za nje katika mwezi huo pia yakiongezeka kwa asilimia 8.2. Maisha ya kawaida yamerejea nchini China, na watu wameanza kula mikahawani na hata kufanya utalii.

Ikiwa nchi iliyochangia maendeleo ya uchumi wa dunia kwa asilimia 30 kwa miaka mingi, kufufuka kwa uchumi wa China kumetia nguvu kwa uchumi wa dunia.

Huu ni mwaka muhimu kwa China, ambapo China itatimiza lengo la kutokomeza umaskini uliokithiri, na kumaliza kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote. Maazimio yatakayotolewa kwenye Mikutano hiyo miwili ya kisiasa ya China si kama tu yatahimiza maendeleo ya uchumi wa China, bali pia yatatia nguvu katika kutuliza uchumi wa dunia nzima.