Waziri wa mambo ya nje wa Marekani anavuruga uhusiano kati ya China na Marekani
2020-05-21 20:33:01| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitoa salamu za kumpongeza Tsai Ing-wen kwa kuapishwa kuwa kiongozi wa Taiwan, akimwita rais wa Taiwan, na kusema uhusiano kati ya Marekani na Taiwan ni wa kiwenzi. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, Pompeo amekuwa kirusi cha kisiasa kinachovuruga uhusiano kati ya Marekani na China.

Tahariri hiyo inasema, hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani kupongeza wazi kuapishwa kwa kiongozi wa Taiwan katika miongo kadhaa iliyopita. Kitendo hicho kimekiuka kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani na taarifa tatu za pamoja zilizotolewa na China na Marekani, na kuonesha kuwa Pompeo ni mwanasiasa anayezingatia maslahi ya kisiasa.

Kwa muda mrefu uliopita, baadhi ya wanasiasa wa Marekani wamechukulia suala la Taiwan kama ni "kadi" ya kuzuia maendeleo ya China. Wakati serikali ya Marekani imeshindwa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, wanasiasa hao wamechukua hadi hiyo tena ili kukwepa wajibu wao.

Akiwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, badala ya kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na virusi hivyo, Pompeo amechukulia majukwaa ya kimataifa ya kidiplomasia kama ni sehemu ya kuipaka matope China bila ya kisingizio chochote.