"Mzozo wa Chama cha Kikomunisti cha China unaota miongoni mwa wananchi", "Kushikilia wazo la kujiendeleza kwa kutoa kipaumbele kwa wananchi"… Wakati wa Mikutano Miwili iliyofanyika nchini China, rais Xi Jinping alipowasiliana na wajumbe waliohudhuria mkutano huo alitaja mara nyingi kutoa kipaumbele kwa wananchi, hali ambayo imeonesha moyo wa kiongozi wa juu wa China wa kuzingatia wananchi.
"Je, kipaumbele kwa wananchi ni nini? Wahudumu wa afya kumhudumia mgonjwa mmoja kumeonesha moyo huo, si ndiyo?" Rais Xi aliuliza. Mjumbe wa Bunge la Umma la China kutoka Mkoa wa Wuhan alipohojiwa na waandishi wa habari alisema, wagonjwa zaidi ya elfu tatu wa COVID-19 waliotibiwa mkoani Hubei wana umri wa miaka zaidi ya 80, kati ya wazee hao, mmoja mwenye umri wa miaka 87 alitunzwa na wahudumu zaidi ya kumi kwa siku kadhaa, na kuondoka katika hali ya hatari. Hali hii iliacha kumbukumbu kubwa kwa rais Xi. Pia amesisitiza tena kuwa inapaswa kutekeleza wazo la kujiendeleza kwa kutoa kipaumbele kwa wananchi wakati wa kuandaa mipango na kutekeleza kazi mbalimbali.
Mwezi Machi wakati janga la COVID-19 lilipoenea kwa kasi mjini Wuhan, mkoani Hubei, rais Xi alifanya ukaguzi mjini humo akisisitiza kuwa inapaswa kuhakikisha maisha ya kimsingi ya wananchi, na kutoa agizo la kuwapatia wakazi wa kitoweo cha samaki kutokana na kuwa ni kitoweo kinachopendwa sana na wakazi wa huko.
Mbali na hayo, maendeleo ya uchumi vilevile yanafuatilia maslahi ya wananchi. Kutokana na athari mbaya zinazoletwa na janga la COVID-19, "kuhakikisha hali ya kimsingi ya kiuchumi, huku ikihakikisha kiwango cha kimsingi cha maisha ya wananchi" ni kazi kuu kwa mambo ya uchumi wa China kwa hivi sasa. Rais Xi aliposhiriki kwenye Mkutano wa wajumbe wa mambo ya uchumi wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa, alizungumzia kuhusu hali ya uchumi ya China na sifa bora ya China, akisisitiza kuwa inatakiwa kuchunguza hali ya hivi sasa ya uchumi kwa mtizamo wa pande zote na kuzingatia siku za baadaye, na kutafuta fursa mpya katika migogoro. Hayo yameonesha wazo la kimkakati wa kiongozi mkuu wa China, ambaye ametoa mikakati kuhusu kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa hatua madhubuti.