Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ni tishio kweli kwa nchi za Ulaya
2020-06-02 21:03:10| CRI

Ingawa Marekani inakabiliwa na maambukizi ya virusi vya Corona na maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi, lakini waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo ambaye ni "waziri mbaya zaidi wa mambo ya nje wa Marekani katika historia" bado hajaacha kutoa kauli zisizo na msingi, akisema China inaharibu maslahi ya Marekani na wenzake wa Ulaya, ambao wanapaswa kushirikiana kupinga China. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, Pompeo ni tishio kwa nchi za Ulaya.

Ikiwa nchi yenye nguvu zaidi duniani, Marekai imeshindwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, na kushuhudia vifo vya watu zaidi ya laki moja kutokana na virusi hivyo. Ili kuzima maandamano yaliyosababishwa na kifo cha George Floyd aliyeuawa na polisi mzungu, kiongozi wa Marekani ametishia kutumia majeshi.

Tahariri hiyo inasema, watu wa Ulaya wanafahamu vizuri Pompeo amefanya nini wakati dunia inakabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Alidai wagonjwa wengi nchini Marekani wanatoka nchi za Ulaya, na kupiga marufuku watu wa Umoja wa Ulaya kuingia nchini humo, alitoa kauli isiyo na ukweli kwamba Jumuiya ya Macho Matano imepata ushahidi wa kuthibitisha kuwa virusi vya Corona vinatoka maabara ya Wuhan, na alikataa kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kuchangia juhudi za kukabiliana na virusi hivyo ulioandaliwa na Umoja wa Ulaya.

Hojaji zilizofanywa na Shirika la Ulaya zinaonesha kuwa, baada ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona, asilimia 73 ya Wajerumani hawakubaliana na Marekani, huku Waitalia wanaoiunga mkono Marekani walipungua na kuwa asilimia 17 tu.

Watu wa Ulaya wametambua kuwa wanasiasa wa Marekani wanazingatia tu maslahi yao ya kisiasa na hawajali nchi za Ulaya, kwani katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imezitatiza sana nchi hizo katika masuala ya biashara, nishati, sayansi na mengineyo. Hali hii inaonesha kuwa Marekani si mwenzi wa kuaminika wa nchi za Ulaya, na wanasiasa wa Marekani haswa Pompeo wanazichukulia nchi hizo kama ni ngazi ya kutimiza lengo la "Marekani kwanza".