Kutoa kipaumbele zaidi kwa watu ni uzoefu mkuu wa China katika kukabiliana na COVID-19
2020-06-08 09:58:27| CRI

Serikali ya China jana ilitoa waraka wa Kampeni ya China ya kukabiliana na COVID-19, ikirekodi mchakato mgumu uliopitiwa na watu wa China katika kupambana na ugonjwa huo, na kutoa uzoefu wenye ufanisi wa kukinga virusi na kutibu wagonjwa, na watu kupewa kipaumbele zaidi.

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza ulioenea kwa kasi zaidi na kuathiri sehemu nyingi zaidi, na pia ni vigumu zaidi kukingwa na kudhibitiwa tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Ikiwa nchi yenye watu bilioni 1.4, kwa nini China imefanikiwa kudhibiti ugonjwa huu kwa haraka? Waraka huo unajibu kuwa, sababu kuu ni uongozi imara wa Chama cha kikomunisti cha China. Tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona, rais Xi Jinping amesisitiza mara nyingi kutoa kipaumbele kwa usalama wa maisha na afya ya watu, akiongoza, kupanga na kuelekeza hatua muhimu za kukabiliana na virusi hivyo.

Maisha ya watu ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine. Waraka huo unasema, kutoka mtoto mchanga mwenye umri wa saa 20, hadi mzee mwenye umri wa zaidi ya miaka 100, China imejitahidi kadiri iwezavyo kumwokoa kila mgonjwa. Kwa mfano, mgonjwa mmoja mwenye umri wa miaka zaidi ya 70 aliendelea kutibiwa na madaktari zaidi ya 10 kwa makumi ya siku, na matibabu kwake yaligharimu dola za kimarekani zaidi ya laki 2.1, ambazo zote zililipwa na serikali. Takwimu zinaonesha kuwa mkoani Hubei, wagonjwa zaidi ya 3,000 wenye umri zaidi ya 80 na 7 wa miaka zaidi ya 100 mkoani Hubei wamepona baada ya kutibiwa vizuri. Balozi wa Iran nchini China Bw. Mohammad Keshavarzzadeh amesema wazo la serikali ya China kutoa kipaumbele zaidi kwa watu linagusa sana hisia. Mtaalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Siasa na Uchumi ya Serbia Bibi Ivona Ladjevac, amesema serikali ya China imezingatia usalama wa maisha ya watu, na kufanya juhudi zote kadiri iwezavyo.

Kila kitu kinategemea watu na ni kwa ajili ya watu. Waraka huo pia umejumuisha uzoefu wa China katika kurejesha uzalishaji baada ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, yaani kudumisha utulivu wa jamii, na kuifanya iendelee kwa utaratibu, na kuhimiza kurejea kwa uzalishaji na maisha ya kawaida ya watu hatua kwa hatua. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili, zaidi ya asilimia 99 ya makampuni makubwa yalikuwa yamerejesha uzalishaji.

Baada ya kushinda virusi vya Corona, watu wa China wanakiamini zaidi Chama cha Kikomunisti cha China na mfumo maalumu wa kisiasa wa China. Sasa wana imani zaidi kwamba, China itashinda changamoto yoyote na kutimiza malengo mbalimbali ya maendeleo, na pia itaendelea kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya dunia.