Muungano wa Haki za Raia wa Marekani wasema ni wakati wa nchi hiyo kuacha kutumia vigezo viwili vya kibinadamu
2020-06-11 20:52:04| CRI

Barua iliyoandikwa na Muungano wa Haki za Raia nchini Marekani kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa imesema, ni wakati kwa Marekani kuchunguzwa na kuhukumiwa, kama ilivyofanya kwa nchi nyingine." Kwenye barua hiyo, muungano huo unautaka Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma za polisi wa Marekani kukandamiza waandamanaji kwa mabavu, pia unasisitiza kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa kuunga mkono matakwa ya jamii ya Marekani kuiwajibisha nchi hiyo kutokana na vitendo vyake vya kukiuka haki za binadamu.

Katika siku kadhaa zilizopita, kifo cha mmarekani mwenye asili ya kiafrika George Floyd kilizusha kampeni kubwa ya haki za binadamu. Uchunguzi wa maoni ya raia uliofanywa kwa pamoja na vyombo vya habari vya Marekani Wall Street Journal na NBC umeonesha kuwa, asilimia 80 ya wamarekani wanaona kuwa nchi hiyo inapoteza udhibiti.

Hata hivyo watekelezaji wa sheria wanaendelea kufanya matukio mbalimblai ya kukiuka haki za binadamu, kwa mfano, huko Virginia, mwanamume mwenye asili ya kiafrika alishambuliwa kwa umeme alipokamatwa, na polisi wa Ohio waliwamwagia waandamanaji pilipili na kuondoa barakoa zao kwa njia za kimabavu, na waandishi wa habari zaidi ya 200 walikamatwa wakati wa kufanya maandamano.

Jambo linalosikitisha watu ni kuwa, baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari hazijikosoa vitendo hivyo na kufanya mikwaruzano ya kikabila kwenye jamii ya Marekani luwa mibaya zaidi.

Miaka 50 imepita tangu Sheria ya haki za kiraia ambayo inapiga marufuku ubaguzi wa rangi kutekelezwa nchini Marekani, serikali ya Marekani haijapata ufumbuzi wa kutatua suala hilo, hata baadhi ya maofisa wa serikali wanachochea na kuelekeza vitendo vya ubaguzi wa rangi, hatua ambayo si kama tu inadhalilisha haki za binadamu, pia inaisikitisha jamii ya Marekani.