Sheria ya usalama wa taifa ni fursa ya kurejesha utulivu kwa Hong Kong
2020-06-16 19:30:36| CRI

Kongamano la kimataifa la kuadhimisha miaka 30 tangu kutolewa kwa sheria ya kimsingi ya Hong Kong limefanyika mjini Shenzhen, China, na kuwashirikisha takriban wataalam 200 kutoka China bara, Hong Kong, Macao, pamoja na Russia, Uingereza, Ujerumani, Hispania na India. Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa tahariri, likisema sheria hiyo itatoa fursa kwa Hong Kong kumaliza vurugu na kurejesha utulivu.

Anthony Carty kutoka Uingereza amesema, vurugu zilizotokea mkoani Hong Kong tangu mwaka jana zimezidi uwezo wa polisi wa mkoa huo, hivyo sheria hiyo ni chaguo la lazima, ili kurejesha utulivu. Wajumbe wengine wanaona kuwa, wakati usalama wa taifa unakabiliwa na tishio kubwa, sheria ya usalama wa taifa itaendeleza mfumo wa "Nchi Moja, Mifumo Miwili", na kuleta uhai mpya kwa mkoa wa Hong Kong.

Wakazi wa Hong Kong pia wameeleza kuunga mkono sheria hiyo. Watu wa hali mbalimbali mkoani humo wameanzisha Chama cha Kuunga Mkono Sheria ya Usalama wa Taifa, na kukusanya saini ya watu milioni 2.93 ndani ya siku nane.

Kutokana na kuanzishwa kwa sheria hiyo, utulivu unarejea mkoani Hong Kong, na mazingira ya kisheria na kibiashara yanaboreshwa siku hadi siku. Hong Kong itakuwa na mustakabali mzuri.