Mapendekezo ya China yaelekeza ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na COVID-19
2020-06-18 19:54:35| CRI

Mapendekezo yaliyotolewa na rais Xi Jinping wa China katika mkutano maalum wa kilele kati ya China na Afrika kuhusu ushirikiano wa kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 uliofanyika jana kwa njia ya video hayo yameelekeza ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na virusi vya Corona.

Katika hotuba yake, Rais Xi amependekeza kushirikiana kukabiliana na ugonjwa huo, kusukuma mbele ushirikiano kati ya China na Afrika, kutekeleza utaratibu wa pande nyingi, kuhimiza urafiki kati ya China na Afrika, na kujenga kwa pamoja jamii yenye hatma ya pamoja.

Kufanyika kwa mkutano huo si kama tu kumeonesha nia ya China ya kutimiza ahadi yake ya kuwa karibu zaidi na Afrika, bali pia kumeonesha imani na nia ya China ya kulinda utaratibu wa pande nyingi, na kuchangia ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na virusi vya Corona.

Mapendekezo ya rais Xi yamepongezwa na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika. Waziri wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa wa Zimbabwe Sibusiso Moyo anaona kuwa, mkutano huo umepata mafanikio makubwa, na kuthibitisha uungaji mkono imara wa China kwa maendeleo ya uchumi na jamii barani Afrika. Mwanahabari wa Gazeti la Alkhabar Alyoum la Misri Fatma Badawy amesema, rais Xi kuahidi kupunguza madeni ya nchi za Afrika, na kuzisaidia kuongeza uwezo wa kukinga magonjwa, kunathibitisha tena kuwa, China imebeba majukumu mapya ya kimataifa.