Marekani imejaribu kufunga mtandao wa kijamii wa China katika nchi za nje "TikTok" kwa kisingizio cha usalama wa nchi, hali ambayo imefuatiliwa sana na watu.
Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuwa, TikTok inapaswa kuuzwa Marekani kabla ya 15 Septemba, ama sivyo itafungwa kwa lazima, akidai kuwa TikTok inatakiwa kulipa malipo makubwa kwa hazina ya Marekani. Msimamo huo wa umwamba umelaaniwa na wamarekani na jamii ya kimataifa.
Aliyekuwa mshauri mwandamizi wa sheria wa Idara ya kupambana na Ukiritimba kwenye Wizara ya Sheria ya Marekani Gene Kimmelman ameeleza kuwa, kauli ya rais wa Marekani haina msingi wowote kwenye Sheria ya kupambana na Ukiritimba. Profesa wa sheria kwenye Chuo Kikuu cha Stanford Mark Lemley pia amedhihirisha kuwa, hakuna ushahidi wa wazi unaoonesha kuwa TikTok inatishia usalama wa Marekani. Vyombo vya habari vya nchi za magharibi pia vinaona kuwa "Usalama wa Taifa" ni uhalifu unaobuniwa na Marekani kwa ajili ya kupambana na makampuni ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu ya China na kuzusha mapambano ya sayansi na teknolojia dhidi ya China.
Gazeti la Financial Times la Uingereza limeeleza kuwa, maingiliano ya serikali ya Marekani ni mbinu inayolenga kuilazimisha kampuni ya China kuiuzia Marekani shughuli za TikTok kwa bei ya chini.
Wachambuzi wa nchi za magharibi wanaona kuwa, ni hatua yenye nia mbaya kwa Marekani kuchanganya madhumuni yake ya kisiasa ya kupambana na China na kutafuta maslahi ya kiuchumi kwa kupata nafasi ya kushikilia soko.