Mauzo ya moja kwa moja mtandaoni yaonyesha mwujiza wa soko la China
2020-11-09 09:42:37| CRI

Kwa mara nyingine tena Wachina wameonyesha uwezo mkubwa wa manunuzi, haswa kupitia mauzo ya matangazo ya moja kwa moja kwenye mtandao wa Internet.

Bw. Zheng Junjie mfanyabiashara wa mvinyo wa Hispania nchini China alisema, wameuza bidhaa za dola laki 5 za kimarekani ndani ya dakika 3 tu hata hivyo alisema awali alidhani kwamba labda ni kosa la kompyuta. Dola laki 5 ni sawa na thamani ya mauzo ya mwaka mzima. China ni soko la mwujiza kweli. Katika maonyesho ya bidhaa ya Shanghai yanayofanyika nchini China, chupa laki 2 za mvinyo zilizoletwa na Bw Zheng ziliuzwa zote Jumamosi jioni kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandanoni.

Katika matangazo yaliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la China CMG peke yake, bidhaa zenye thamani ya dola milioni 20 kutoka nchi mbalimbali ziliuzwa zote kupitia mtandao. Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa China kufanya Maonyesho ya Uagizaji bidhaa kutoka nje ya Shanghai, na kutokana na mbinu hiyo mpya ya mauzo yanayopamba moto, watu wanaweza kununua bidhaa hizo wakikaa nyumbani. Kwa mujibu wa ripoti ya kampuni ya uchunguzi wa data ya Nielsen, mwaka huu karibu nusu ya wateja wa China, ambayo ni watu milioni 265 wananunua bidhaa katika matangazo ya moja kwa moja mtandanoni.

Katika miaka ya karibuni, bishara ya nchini imekuwa injini ya kwanza ya ukuaji wa uchumi wa China, mwaka jana ilichangia asilimia 57.8 ya ongezeko la pato la taifa la China. Inakadiriwa kuwa katika miaka 10 ijayo, China itanunua bidhaa kutoka nje zenye thamani ya dola trilioni 22 za kimarekani. Nchi hiyo yenye watu bilioni 1.4, ambayo watu milioni 400 ni wenye mapato ya wastani, ni nguvu kubwa ya kuwavutia wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali. Soko hilo kubwa si kama tu linasaidia ukuaji wa uchumi wa China, bali pia linahitaji bidhaa nyingi za nchi za nje, hivyo kutengeneza fursa nyingi za maendeleo duniani na kuwapa watu moyo na matumaini hususan wakati tunakabiliwa na changamoto zinazoletwa na maambukizi ya virusi vya Corona.