Daraja la juu la Kijazi lililojengwa na kampuni ya ujenzi ya China CCECC mjini Dar es Salaam limezinduliwa rasmi.
Akizindua daraja hilo jana Jumatano, Rais John Magufuli wa Tanzania amewashukuru wajenzi wa China na Tanzania kwa kukamilisha mradi huo kwa wakati, na kusema daraja la Kijazi litapunguza kidhahiri msongamano wa magari barabarani mjini Dar es Salaam, na pia litarahisisha usafiri wa wakazi wa mji huo.