Mwadui wasema walifungwa kwa kuwa walikuwa ugenini, nyumbani ingekuwa tofauti
2021-04-19 18:47:40| cri

Kocha Mkuu wa klabu ya Mwadui FC Salhina Mjengwa amesema kama wachezaji wa Simba wangekuwa upande wake basi ingekuwa rahisi kushinda mchezo wa jana Aprili 18 mbele ya Simba. Mwadui FC iliyo nafasi ya 18 na pointi 16 ilipoteza mbele ya Simba kwa kufungwa bao 1-0 na kuwafanya waziache pointi sita jumlajumla kwa wapinzani hao msimu huu wa 2020/21. Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru ubao ulisomeka Simba 5-0 Mwadui na jana pia walipoteza kwa bao la ushindi lililofungwa na nahodha mzawa, John Bocco. Amesema wachezaji walikuwa walitengeneza nafasi lakini ilikuwa vigumu kuzibadili kuwa goli, hata hivyo bado wana mechi mbele ambazo anaamini kuwa wanaweza kufanya vizuri.