Sheria mpya ya kukinga magonjwa ya wanyama yatangazwa nchini China
2021-04-21 12:43:22| Cri

Katika miaka ya hivi karibuni, hatari zinazosababishwa na kutembea na mbwa bila kutumia kamba zimetokea mara kwa mara. Ili kukabiliana na tatizo hilo, “Sheria mpya ya kukinga magonjwa yanayosababishwa na wanyama” iliyoanza kutekelezwa tarehe 1 Mei mwaka huu, imesema wazi kuwa inapaswa kuweka kipande cha kitambulisho cha mbwa na kuweka kamba shingoni mwa mbwa wakati wa kutembea na mbwa, ili kuzuia mbwa kuwaumiza watu na kueneza magonjwa.

Sheria hiyo pia imesema wazi kuwa, watu watakaokiuka sheria kama hizo, watatozwa faini chini ya RMB yuan elfu moja, sawa na dola za kimarekani 150, na wale ambao hawajirekebishi makosa yao ndani ya muda uliowekwa, watatozwa faini kati ya yuan 1000 na 5000, sawa na dola za kimarekani kati ya 150 na 770.