China yadumisha kinga ya COVID-19 katika Mlima Qomolangma
2021-05-10 18:38:47| Cri

China inaendelea kuchukua hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona katika Mlima Qomolangma, na mpaka sasa hakuna kesi zozote za maambukizi zilizoripotiwa tangu kuanza kwa msimu wa kupanda mlima huo mapema mwezi April.

Hayo yamesemwa na maofisa waliozungumza na Shirika la Habari la China Xinhua katika mkutano wa kupambanba na mlipuko uliofanyika hivi karibuni katika kambi iliyoko chini ya mlima huo.

Shirikisho la Wapandamlima la Tibet nchini China (CTM) limesema, vibali 21 vya kupanda mlima vimetolewa kwa raia wa China mwaka huu katika upande wa kaskazini wa Mlima, na kuongeza kuwa hakuna raia wa kigeni walioruhusiwa kuingia eneo la Qomolangma tangu mlipuko wa virusi vya Corona ulipotokea mwaka jana.