Kampuni 42 zasaini mkataba wa kushiriki kwenye maonyesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa za matumizi
2021-05-10 19:21:54| CRI

Kampuni 42 zimesaini mkataba wa kushiriki kwenye maonyesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa za matumizi CICPE, ikiwemo kampuni ya Tapestry ya Marekani, kampuni ya ETRO ya Italia na kampuni ya kimataifa ya ushauri ya Deloitte.

Kwa mujibu wa waratibu wa maonyesho hayo, kampuni hizo zinatoka kwenye sekta za huduma za maisha yenye mitindo ya kisasa, huduma za utalii, matumizi ya huduma, chakula na bidhaa za afya, na vito vya mapambo.